Na Amiri kilagalila,Njombe

Kijana anayefahamika kwa jina la Chesco Mtega mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kitongoji cha Kanisa A Kijiji cha Ludewa,wilayani Ludewa mkoani Njombe amegundulika amejinyonga kwa kutumia shuka lililofungwa juu ya kenchi na shingoni mwake ndani ya nyumba,huku sababu zikitajwa ni kutokana na msongo wa mawazo (SONONA)

Akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake mkuu wa Wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo Mh, Andrea Tsere amesema inadaiwa kijana huyo alichukua uamuzi huo kutokana na kuwa na msongo wa mawazo. 
  
 “Inadaiwa huyu kijana alifanya hivyo kwasababu ya msongo wa mawazo,sijajua alikuwa na historia gani lakini pia inaonekana alikuwa mtundu mtindu zaidi” Alisema Tsere

“Tunaendelea kufanya uchunguzi zaidi ni kwanini hasa amefikia hatua ya kujinyonga,historia yake ikoje,ndugu zake wanaushirikiano gani,anadaiwa nini,kuna mgogoro gani kwenye familia,kwasababu mtu mzima mpaka anafikia hatua ya kujinyonga lazima kuna jambo ndani yake”aliongeza Tsere

Aidha Tsere ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na ndugu wa karibu katika mawazo au changamoto ili kutatauliwa badala ya kukaa kimya na kusababisha matatizo.

“Wito wangu kwa makabila yote ni kuwasihi watu wote wajaribu kushirikiana na ndugu zao,wakubwa zao,wadogo zao katika changamoto walizo nazo ili waweze kutatua badala ya kukaa nazo na baadaye unajinyonga”aliongeza Andrea Tsere

Vile vile ametaka watu kumuomba Mungu atakayeweza kuonyesha njia kwasababu watu wanaofikia hatua ya kujitoa uhai wanakuwa wamejitenga na Mungu kwa muda mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...