MFANYABIASHARA,  Salum Rajabu Selemani (51), anyeishi Kibaha Pwani, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa USD 898,000.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Easter Martin mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Rashid Chaungu imedai kuwa, kati ya Aprili Mosi na 20, mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro  na huku Lubumbashi Congo mshtakiwa akiwa kama mtanzania alifanya udanganyifu kwa Segere Bushiri, Rocky Kungala na Paty Lufunda.

Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alijipatia kiasibcha Sh. 898,000 kwa madai kwamba angezirudisha fedha hizo kwa Albert Makundi Mayombo ambaye yupo jijini Dar es Salaam huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la pili la utakatishaji fedha imedaiwa katika tarehe3hizo gozo huku Turiani Morogoro,  mshtakiwa alijihusisha na muamala wa USD 898,000 huku akijua kuwa fedha hizo ni mazalia ya kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu uchumi

Kwa mujibu wa upade wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na itatajwa tena Julai 7, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...