Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa Wateja wa TMDA kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi katikati akionesha mkataba wa huduma kwa wateja wa TMD kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Erick Shitindi na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo.
Mganga
Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi akizungumza wakati wa uzinduzi
mkataba wa huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)
katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo
akitoa maelezo ya mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Mamlaka hiyo katika
Hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
====== ======= ====== =======
*Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya watakiwa kuwa na mkataba wa huduma kwa wateja.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto imesema Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo zinapaswa kuwa na mkataba wa huduma kwa Wateja ili kurahisisha utoaji wa huduma boara kwa wanannchi.
Hayo ameyasema Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi jijini Dar es Salaam wakati akizindua mkataba wa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), amesema kuwa TMDA imekuwa na mipango mizuri katika utoaji wa huduma kwa kuzingatia muda katika utoaji wa leseni kwa wadau mbalimbali.
Profesa Makubi amesema kuwa TMDA imekuwa na mifumo ya viwango ambapo Shirika la Afya Duniani inatambua pamoja na jumuiya mbalimbali na hiyo inatokana na mikakati ya watendaji wa taasisi waliojiwekea ya kuhakikisha wanakwenda kutatua matatizo ya huduma katika utoaji wa huduma.
Amesema kuwa TMDA inatoa mkataba mara ya nne ambapo amewataka mamlaka hiyo kufuatilia mkataba huo kuona malengo waliojiwekea yameweza kama wameweza waliojipangia pamoja na huduma wanazozitoa kwa wadau.
Nae Kaimu Mkurgenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema kuwa katika mkataba huo wamezingatia muda wa utoaji wa usajili za waingizaji dawa kutoka siku 240 hadi 180 na wa ndani kutoka siku 120 hadi siku 60 na usajili dawa sehemu za biashara kutoka siku 10 hadi 8.
Fimbo amesema kuwa mkataba huo umezinagatia maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma na kuleta ufanisi pamoja na kuweka mikakati kuendelea kutoa huduma bora
kwa wadau amesema TMDA tangu walipoanza kutengeneza mkataba wa huduma kwa wateja wamekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma bora kutokana na watendaji kujipanga katika kuhudumia wateja hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...