Na Mwandishi Wetu, Arusha

WATU tisa wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Mkoa wa Arusha wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushes( TAKUKURU) mkoani humo kwa tuhuma mbalimbali za rushwa.

Taarifa ya TAKUKURU Mkoa wa Arusha imesema kuwa watu hao imewakamata katika nyakati tofauti ambapo wamo pia watumishi wa Serikali na wafanyabiashara.

Imewataja watu hao wanaotuhumiwa kwa rushwa ni Sifael Palangyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM, Upendo Ndorosi ambaye ni Katibu wa Malezi Wilaya ya Longido na Mjumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Arusha na Laraposho Laizer ambaye ni Katibu wa Wazazi Wilaya ya Longido.

Wengine ni Godwait Mungure ambaye ni Katibu wa Wazazi kata ya Kikatiti Meru, Mboiyo Mollel ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Tukusi kata ya
Loksare wilayani Monduli,Mikidadi Mollel ambaye ni Mwenyekit wa Kamati ya Pembejeo kijiji cha Tukusi, Kanankira Mnyari ambaye ni Wakala wa pembejeo za kilimo kijiji cha Loit kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Gervas Mollel mfanyabiashara wa Kata ya Oltrumet wilayani Arumeru pamoja na Joseph Christopher Mollel mfanyabiashara katika Kata ya Oltrumet.

Kuhusu makosa wanayotuhumiwa nayo, taarifa hiyo ya TAKUKURU imefafanua kuwa Juni 26 mwaka huu ilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema Lilian Ntoro ambaye anatarajia kugombea ubunge wa Viti Maalum Wazazi Mkoa wa Arusha alikuwa amempatia fedha Sifael Pallangyo kwa ajili ya kwenda kuwahonga wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi Walaya ya Longido ili kushawishi cha kumpigia kura katika kura za maoni.

"Baada ya kupokea taarifa hiyo TAKUKURU Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Longido ambao waliandaa mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kila mmoja akiwa na kiasi tofauti cha fedha zilizokuwa zimeandaliwa kugawiwa kwa wajumbe wa baraza la wazazi jumuiya ya Wilaya ya Longido,"imesema.

Pia taarifa hiyo imeeleza katika kosa la pili TAKUKURU inawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Gervas Andrea Mollel na Joseph Christopher Mollel wote ni wafanyabiashara wa Kata ya Oltrumet kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh.milioni 15 kutoka kwa mfanyabiashara mwenzao Advera Kyaruz mkazi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...