Mkazi wa Dodoma, Fredrick Nachipyangu(40) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka mawili, likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh. Milioni 33.
Mshtakiwa Nachipyangu, amesomewa mashtaka yake leo Juni 10, 2020 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Kasian Matembele.
Imedaiwa kuwa, April 24, 2015 huko katika benki ya CRDB tawi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa kwa njia ya udanganyifu alijipatia USD 14,320 kupitia account yake binafsi kutoka Kampuni ya Changshu Menglan Imp and Exp Co.vide baada ya kujifanya kuwa ni mhasibu wa kampuni ya Kirobe Investment Co.Ltd na kwamba fedha hizo zinatakiwa zitumike kununua ngozi za wanyama, jambo ambalo sio kweli.
Katika shtaka pili, imedaiwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa huyo alitakatisha kiasi cha USD14, 320 sawa na Sh. Milioni 33 kutoka Kampuni ya Changshu Menglan Imp and Exp Co.vide, wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udangangifu.
Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za hiyo. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali Juni 22, 2020.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...