Mmoja ya viongozi wa waendesha bodaboda katika
Jiji la Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi baada ya kudaiwa kuvuruga mkutano
ambao ulikuwa umeitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.Kiongozi
huyo anadaiwa alitoa taarifa za kuhairisha mkutano huo jambo ambalo halikuwa
limewafurahisha wengine.
Askari Polisi wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi
mmoja ya viongozi wa waendesha bodaboda baada ya kutuhumiwa na waendesha
bodaboda wenzake kuwa ametangaza kuhairishwa kwa mkutano kati yao na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.
Mmoja ya waendesha bodaboda akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kutokea kwa sintofahamu ya kuhairishwa kwa mkutano kati ya
wanedesha bodaboda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa katika
viwanja vya Leaders baada ya mkutano kati yao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
kuharishwa na kuzua sintofahamu.
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MKUTANO kati ya wamiliki na waendesha bodaboda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam umeshindwa kufanyika katika Viwanja vya Leaders jijini na hakukua na sababu maalum ya kutofanyika kwa mkutano huo.
Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huo ulipangwa kuanza saa tatu asubuhi ya leo Juni 9,2020 lakini hadi saa saba mchana mkutano huo ulikuwa bado haujafanyika.
Wakati wamiliki na waendesha bodaboda na bajaji wakiendelea kuingia kwenye viwanja, pia kulikuwa na wageni waalikwa ambao walikuwa wamekuja kufuatilia mkutano huo.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye aliyekuwa akisubiriwa.
Baadae kidogo baadhi ya waendesha bodaboda walionekana wakielekea eneo moja na dakika chache tu kukazuka vurugu na malumbano baina yao.Walikuwa wakilalamikiana kuvuruga mkutano kiasi cha mmoja wao kulazimika kuchukuliwa na askari polisi baada ya kuonekana akishambuliwa na wenzake.
Polisi waliokuwa eneo hilo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo hilo la mkutano waliamua kumchukua huyo anayedaiwa kuwa kiongozi na kisha kumuingiza kwenye gari lao na kuondoka naye.
Wakizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog baadhi ya waendesha bodaboda wameeleza kushangazwa kutofanyika mkutano huo na hakukua na sababu yoyote ambayo wameelezwa zaidi tu ya kushuhudia wenyewe kwa wenyewe wakivutana.
Seleman Farijala ambaye ni moja ya waendesha bodaboda amesema kuvurugika kwa mkutano huo ni aibu kwao na kuongeza walitarajia kwenye mkutano huo na Mkuu wa Mkoa watoe malalamiko yao ambayo mengi na yanawasababishia wenyewe kwa wenyewe.
"Huu mkutano wa leo ulikuwa muhimu sana kwetu, tulitarajia Mkuu wa Mkoa aje tuzungumze naye na kumueleza changamoto zetu ambazo ni nyingi, hata hivyo kuna wenzetu wameamua kuuvuruga lakini sisi bado tunataka kukutana na Makonda tumueleze changamoto tulizonazo,"amesema Farijala.
Omari Kimbaula ambaye naye ni mwendesha bodaboda jijini Dar es Salaam amesema hata kama mkutano wao na Mkuu wa Mkoa haujafanyika lakini wanaimani watapata nafasi ya kukutana naye na kuzungumza yanayowasibu huku akihoji sababu za leo mkutano kutofanyika.
Hata hivyo mmoja ya makada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) aliyekuwa akizungumza na askari polisi waliokuwa eneo hilo alisikika akisema mkutano huo umeahirishwa baada ya kufanya mawasiliano na Mkuu wa Mkoa na kwamba utafanyika siku nyingine Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Pamoja na maelezo hayo haikufahamika moja kwa moja sababu za kuahirishwa kwa mkutano huo ingawa sababu kubwa ilionekana kutoelewana kwa vyama vya waendesha bodaboda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...