Na mwandishi wetu, Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Idd Hassan Kimanta amesema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) una faida kubwa kwa Wafanyakazi, Waajiri na Taifa kwa ujumla kwa vile Wafanyakazi sasa wana kinga ya kipato hata kama watapatwa na ajali, magonja kutokana na kazi.


Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2020 katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Laban Kihongesi wakati akifungua mafunzo ya uelimishaji wa tathmini za ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kwa madaktari na
watoa huduma ya afya wa kanda ya kaskazini, yanayofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC jijini Arusha.


“Hivi sasa wafanyakazi wanauhakika wa kinga ya kipato kutokana na majanga yasababishwayo na ajali, magonjwa au vifo kutokana na kazi kutokana na uwepo wa Mfuko huu.” Alisema Kimanta

Aidha waajiri nao wanapata muda zaidi wa kushughulikia masuala ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na kazi zao kwani Mfuko ndio unaobeba mzigo wa gharama pindi mfanyakazi anapoumia, kuugua ama
kufariki kutokana na kazi.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema, faaida nyingine ni kuongezeka kwa pato la Taifa kunakotokana na kukua kwa tija na uzalishaji katika maeneo ya kazi.

“Mtakubaliana nami kuwa, kuanzishwa kwa Mfuko wa Fidia ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi mahiri wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajenga uchumi wa viwanda na hivyo kuwa na ongezeko kubwa la maeneo ya uzalishaji linalokwenda sambamba na ongezeko la matukio na athari zitokanazo na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi.” Alisema Mkuu huyo wa Mkoa. 

Akizungumzia mafunzo hayo, Mhe. Kimanta alisema mafunzo yanalenga kuwawezesha madaktari na wataalamu wa afya kuhakikisha kuwa tathmini hizi za ulemavu zinafanyika kwa usahihi na wafanyakazi walioumia au kuugua wanapata fidia stahiki na kwa wakati.

Mfuko ulianza zoezi hili katika mwaka wa fedha 2015/16 na “Mpaka sasa jumla ya madaktari 956 kutoka wilaya zote nchini wameshapatiwa mafunzo haya na mafunzo ya leo ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Mfuko huu ili kuimarisha utoaji wake wa huduma.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema
Mafunzo haya ya siku 5 yameandaliwa na Mfuko kama sehemu ya hatua muhimu kuuwezesha kutekeleza vyema jukumu la kufanya tathmini sahihi na kwa wakati pindi mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi.


“Tunaamini kuwa uelimishaji wa aina hii ni moja ya mikakati ya kuondoa changamoto ambazo zinaukabili Mfuko mpaka sasa.” Alisema Bw. Mshomba.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano Mfuko umekuwa na mafanikio makubwa na kubainisha kuwa mwaka wa kwanza wa ulipaji fidia Mfuko ulilipa kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na Mfuko unatarajia kulipa kiasi cha shilingi bilion 8.5 mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.

Alisema wawezeshaji wa mafunzo haya ni wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hospitali ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Hospitali ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) ambao wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu sana na Mfuko kuanda miongozo ya tathmini ya ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenan Laban Kihongesi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa hotuba ya kufungua mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenan Laban Kihongesi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa hotuba ya kufungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wakinakili na wengine wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
 Kenan Laban Kihongesi, Mkuu wa Wilaya ya Arusha akipongezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary (kushoto) mara baada ya kutoa hoituba yake.
Meneja wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Skt. Ali Mtulia akifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakiendelea kwenye mkutano huo.
Mgeni rasmi Kenan Laban Kihongesi (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Arusha, akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa AICC jijini Arusha baada ya kufungua mafunzo hayo.
 Kihongozi akiagana na  Mshomba (wakwanza kulia), Dkt. Omary (wapili kulia) na Mkuu wa jopo la wawezeshaji wa Mafunzo hayo Dkt. Robert Mhina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...