MSANII nyota wa
miondoko ya Afro Pop, Pop na RnB kutoka Nchini Nigeria, Adefemi Ebenezer
maarufu kama Olakira Ijumaa ya 26 Juni anatarajia rasmi kuachia wimbo
mpya wa ‘In my Maserati’.
Olakira anayetamba na
nyimbo bora mbalimbali zikiwemo ‘Aya Mi’, ‘Wakanda Jollof na zingine
nyingi ambapo kwa sasa anakuja ba ujio mpya wa wimbo wake utakaokuwa kwa
sauti na video ‘In my Maserati’.
“Wimbo wa In my
Maserati unaelezea namna anavyovutiwa na gari la kifahari aina ya
Maserati akimuahidi mpenzi wake na kuliendesha gari hilo”
Wimbo huo
umetayarishwa na Olakira mwenyewe huku video ikiwa imechukuliwa viunga
vya Jiji la Lagos na kuongozwa na Clarence Peters.
Tazama hapa Video Link: https://www.youtube.com/watch?v=QEPmDnVkLzg&feature=youtu.be
Store Link: smarturl.it/inmymaserati
Aidha, Msanii Olakira
amekuwa akifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Nchini Nigeria na
Afrika kwa ujumla kwa kutoa muziki mzuri wa Afropop.
Ujio wake katika
Afropop alianza na wimbo wa ‘Hey Lover’ na baadae wimbo wa ‘Flirty
signal’ ambapo zilipokewa vizuri na kupata watazamaji (views) wengi
kupitia mtandao wa Youtube.
Olakira pia
ameshiriki kuandika na kuandaa wimbo uliofanya vyema katika Afro wa
‘Akube’ na ‘My Woman’ wa Dotman na kumuweka katika chat za juu kwenye
ramani ya muziki Afrika.
Pia mbali na kuwa ni Mwanamuziki, Olakira ni Mtayarishaji wa muziki (Producer ),mwandishi wa mashahiri ya muziki (songwriter ).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...