MKAZI wa Jiji la Dar es Salaam Pedro Chongo a.k.a Salim Mgana amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye uzito wa gramu 1523.25.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na Wakili wa Serikali Janet Magoho leo Juni 26, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate imedai kuwa, Aprili 9, 2011 huko katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere ndani ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa akisafirisha kilo hizo 1523.25 za Cocaine.
Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 10,mwaka huu. Mshtakiwa amerudishwa rumande.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...