Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka waajiri wote nchini ambao hawawasilishi michango  ya wafanyakazi kujisalimisha mapema wenyewe NSSF kabla ya kuchukulia hatua za kisheria.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa kikao baina ya Menejimenti ya NSSF,Kampuni ya Knight Support na Wafanyakazi wa Knight Support juu ya mustakabali wa malimbikizo ya wasilisho la michango ya wafanyakazi pamoja na tozo ya adhabu inayofikia takribani Tsh 8.4Bn ikiwa ni michango ya kuanzia mwaka 2011-2018.

Katika kikao hicho Naibu Waziri Mavunde alielekeza yafuatayo;

* NSSF ifanye mawasiliano  na Wizara ya Mambo ya Nje juu ya kurejeshwa nchini mmiliki wa Kampuni ya Knight Support Raia wa Uingereza Bi. Christine Sutton

*Mwakilishi wa Kampuni hapa nchini Bw.Blessing Kachambwa raia wa Zimbabwe azuiwe kutoka Nchini mpaka hapo wahusika wakuu wa Kampuni watakaposhughulikia malipo ya malimbikizo ya michango ya wafanyakazi.

*Kwa kuwa NSSF imeshinda kesi mahakamani juu ya deni hilo tajwa hapo juu,na kwa kuwa imethibitika kwamba Kampuni ya Knight Support haina mali za kukamata kuuzwa na kufidia deni, Kurugenzi ya Sheria NSSF iandae nyaraka za kisheria za maombi ya kuwakamata wahusika wakuu na kuwafanya wafungwa wa madai (Civil Prisoners)

*Uchunguzi wa kina ufanyike kubaini wafanyakazi wa NSSF ambao hawakutimiza wajibu wao kwa kutofuatilia michango tangu mwaka 2011-2018.

*NSSF kuandaa orodha ya wadaiwa wote sugu na wale wote wasiowasilisha michango ya wafanyakazi ili zoezi la ufuatiliaji na kuchukua hatua za kisheria kuwapeleka wahusika mahakamani lianze mara moja.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi wa Knight Support (wa kwanza kulia), Bresing Kachambwa na Wahasibu wa kampuni hiyo wakiwa kwenye gari ya Polisi, Makao Makuu ya NSSF baada ya kukamatwa kutokana na kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wa kampuni hiyo inayofikia Tzs. bilioni 8.417.
Mhasibu wa Kampuni ya Ulinzi ya Knight Support (mwenye shati nyeupe aliyekaa) pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bresing Kachambwa (aliyekaa kushoto) wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi, kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa Kituo cha Polisi.
 NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto) akiongoza kikao baina ya Menejimenti ya NSSF na uongozi wa Knight Support.
 Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa NSSF, Bw. Suleiman Msangi (aliyesimama), akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde, taarifa ya kuchelewa kuleta michango kwa Kampuni ya Night Support.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...