Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete ametaka ufafanuzi kuhusu usalama wa mifugo ambayo itakamatwa baada ya kuingia kwenye maeneo ya hifadhi kabla ya kesi kuanza Mahakamani.
Akizungumza leo Juni 10,2020,Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kuchangia muswada wa marekebisha ya sheria mbalimbali ambao umewasilishwa bungeni hapo na moja marekebisho hayo inahusu Wanyamapori na Uhifadhi.
"Kwanza naomba nianze kwa kukupongeza Naibu Spika Dk.Tulia Acksoni pamoja Spika Job Ndugai kwa jinsi ambavyo mnaliongoza na kuliendesha Bunge letu,"amesema.
Amesema sheria ya Wanyampori na uhifadhi ni moja ya eneo ambalo ni muhimili mkubwa na kwa sasa wameondoa utaratibu wa kukamata na kuchukua mifugo."Nina jambo moja kwa Waziri na hili ni kutaa kufahamu Serikali imejipangaje kabla ya kufika mahakamani mifugo inalindwa.Nataka tujue Serikali imejipangaje kuhakikisha mifugo kabla ya kufika mahamaki inakuwa katika hali nzuri".
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...