Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Idd Hassan
Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika hafla fupi iliyofanyika
Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akimuapisha Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wakila kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya uapisho.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi
mbalimbali mara baada ya kumuapisha Idd Hassan Kimanta kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Arusha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
leo tarehe 22 Juni 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa mara baada ya tukio la uapisho Ikulu
jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Idd Hassan Kimanta akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan
Laban Kihongosi Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2020. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta akila kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa.
Picha na Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...