Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wakati wa ziara ya kukabidhi miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Mhe. Paul Makonda wakati wa ziara ya kukabidhi miradi ya maendeo ya jimbo la Kawe na Kinondoni kwa kamati ya siasa ya mkoa huo, mwenyesuti nyeusi ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndug.Aron Kagurumjuli.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni , Mhe. Benjamini Sitta akiwasalimia wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wakati wa zaiara ya kukabidhi miradi ya Maendeleo ya Manispaa hiyo katika Jimbo la Kawe na Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni wakikagua barabara ya Shekilango Mwenge iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

………………………………………………………………………………………….

Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam zimetakiwa kuiga mfano wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali kuu pamoja na wadau kama ilivyotekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kwa jimbo la Kinondoni na Kawe yenye lengo la kukabidhi miradi kwa kamati ya siasa ya Mkoa.

Amesema kuwa kila Halmashauri katika Mkoa wa Dar es Salaam inakusanya mapato hivyo zinapaswa kutekeleza miradi ambayo itaaacha alama kama ambavyo Manispaa ya Kinondoni imeweka alama katika miradi mikubwa ya Maendeleo chini ya Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi mzalendo Ndg. Aron Kagurumjuli.

“Kinondoni nawapongeza sana, mmefanya kazi inayoonekana nakuacha alama kwa Wananchi, kipindi cha nyuma haya mambo hayakuwepo licha ya kwamba Manispaa zilikuwa zinakusanya mapato lakini katika uongozi wa miaka mitano ya Dk. Magufuli mmeitendea haki ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ” amesema Makonda.

Akizungumzia mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, Mhe. Makonda amesema soko hilo lililojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, ni chanzo kikubwa cha mapato katika Manispaa ya Kinondoni litakaloongeza hadhi ya wafanyabishara watakaoendesha shuguli zao bila kubugudhiwa.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Chongolo amesema kuwa katika Wilaya hiyo Mkurugenzi pamoja na timu yake wamefanikiwa kukamilisha miradi kwa wakati na kwamba wanapoikabidhi kwa kamati hiyo inatoa fursa kuendelea kutekeleza miradi mingine.

Chongolo amesema kuwa miradi iliyotembelewa Jimbo la Kawe na Kinondoni ilikuwa ni alama ya kukabidhi miradi hiyo kwa CCM ngazi ya mkoa ikiwa ni baada ya kuikamilishwaji wake na kueleza kuwa soko la kisasa la Magomeni hadi sasa limekamilika kwa asilimia 95 na kwamba hadi kufikia Agosti mwaka huu litakuwa limeanza kutumika na wafanyabiashara.

Katika Ziara hiyo Mhe. Makonda ametembelea miradi mbalimbali ambayo ni ujenzi wa Hospital ya Wilaya iliyopo Mabwepande, Kiwanda Cha kuchakata taka, Shule ya wasichana Mabwe Tumaini na Zahanati ya Bunju.

Miradi mingine ni ujenzi wa matanki ya Maji , ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Shekilango hadi Bamaga, Soko la Kisasa Magomeni, Kituo Cha Afya kigogo, Zahanati ya Mikoroshini ,Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu Mwenge pamoja na Stedi ya daladala iliyopo Mwenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...