Na.Khadija seif, Michuzi tv

  - Rich rich aona Raha ya kuwepo Azam tv, tamthilia 4 madebe na shilingi yake.


KAMPUNI ya Azam media imezindua filamu nne kwa mpigo jijini leo jijini Dar es salaam.

 Akizungumza na Michuzi tv Mtendaji mkuu wa kampuni ya Azam Media, Tido Mhando amesema Sasa ni wakati wa kuwapa burudani za kinyumbani zaidi watazamaji wao.

"Tumekuwa tukipokea malalamiko,maoni na ujumbe kutoka kwa watazamaji wet,u kupitia mitandaoni kuhusu juu ya kutaka kuona tamthilia za kinyumbani na kuona wasanii kutoka hapa nchini hivyo tukaiona haja ya kuwaletea watazamaji wetu kitu wanachotaka na ndio maana tumeamua kuleta tamthilia nne kwa mpigo zilizotengenezwa na kuchezwa na watu maarufu,wakongwe pamoja na wapya kwenye tasnia hiyo,"

Aidha, Mhando amezitaja tamthilia hizo ni pamoja na panguso ya Jimmy Mafufu,single mama ya jb, shilingi ya madebe lidai pamoja ja na tandi ya Ray kigosi zitakazoanza julai 13 saa 3 usiku.

Huku  Mkurugenzi wa Mauzo na masoko sabrina Mohammed akifafanua zaidi kuwa tamthilia hizo zitarushwa kwa kifurushi cha chini kabisa kuanzia  elfu 3 mpaka elfu 10.

Hata hivyo kwa upande wake msanii mkongwe ambae pia ni mmoja wa waandaji wa tamthilia ya "single mama" single Mohammed mtambarike a.k.a Rich amesema ni wakati wa kuifufua tasnia ya filamu na kuleta mapinduzi ya kiburudani zaidi.

"Bado tunaona mchango wa kuendelea kuwepo kwa wadau kama azam tv na wengine ni wazi tasnia inahitaji kufika mbali na kufikia soko la kimataifa ,"

Pia ametoa pongezi kwa uongozi wote wa Azam tv kwa kubeba dhima ya kuonyesha tamthilia hizo za kiswahili na kukusanya wasanii wa kinyumbani.

 Mtendaji mkuu wa Azam media  Tido Mhando Akizungumza na waandishi wahabari waliohudhuria katika uzinduzi wa tamthilia nne za kitanzania shilingi,single mama,panguso na Tandi
 Mkurugenzi wa Mauzo na masoko Sabrina Mohammed akiteta Jambo pamoja na Mtendaji mkuu wa Azam media Tido Mhando wakati wa uzinduzi wa tamthilia nne zitakazorushwa hivi karibuni kupitia azam tv
 Wasanii mbalimbali akiwemo Eshe Buheti,Maya,Mzee kikoti,Monalisa na wengine waliohudhuria katika uzinduzi wa tamthilia nne zitakazorushwa na Azam media  jijini Dar es salaam
 Wasanii mbalimbali akiwemo eshe buheti,Maya,mzee kikoti,monalisa na wengine waliohudhuria katika uzinduzi wa tamthilia nne zilizozinduliwa na Azam media  jijini Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...