-WALIOREJESHA FOMU WAFIKIA WANNE

NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR.

WANAMAMA wawili  wamejitokeza leo 24 Juni kuchukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar  kupitia tiketi ya Chama  Cha Mapinduzi CCM.

Mwanamama wa kwanza ni Husna Attai Masoud aliwasili viwanja vya Afisi Kuu ya CCM -Zanzibar  zilizopo eneo la  Kisiwandui majira ya saa Nne akiwa amesindikizwa na wapambe wake watano wote  Wanamama akiwemo dereva aliyewaendesha na

kisha kupanda hadi gorofa ya pili kwa Katibu wa Idara ya Organization CCM, Zanzibar, Cassian Galos na kukabidhiwa fomu hiyo inayolipiwa Milioni moja.

Hata hivyo Mwanamama huyo hakuwa tayari kuzungunza na Wanahabari zaidi aliwaomba kufanya hivyo mara tu atakapokamilisha taratibu za wadhamini.

"Nashukuru sana uwepo wenu Wanahabari. Kwa sasa muda ni mdogo hivyo nakimbizana na muda ili niwahi kutafuta wadhamini na kurejesha. Nitakaporesha titaongea mengi zaidi" Alieleza Husna Attai Masoud.

Kada wa pili ni Mwanamama, Fatuma Kombo Masoud ambaye aliwasili majira ya saa Sita na nusu akiwa na mpambe mmoja ambapo waliingia kwa miguu ndani ya viunga vya Afisi kuu ya CCM -Zanzibar tofauti na wagombea wengine ambao wamekuwa wakiingia kwa magari.

Hata hivyo Fatuma hakuwa tayari kuzungumza zaidi aliwaomba Wanahabari akapitie kwanza fomu kisha atapata wasahaa baada ya kurejesha.

Husna Attai Masoud na Fatuma Kombo Masoud wanakuwa makada wa tatu baada ya mwanamama, Mwatum Mussa Sultan  kuchukua 19 Juni.Mwitikio wa Watia nia Wanamama imekuwa ya msukumo mdogo visiwani hapa kujitokeza kugombea nafasi hiyo nyeti ya Urais.

Aidha hadi sasa waliokwisha kujitokeza kurejesha fomu ni pamoja na Balozi Ali Karume, Mohammed Hija Mohammed, Mbwana Bakari Juma na Abdulhalim Mohammed Ali.Aidha hadi sasa watia nia wengine waliokwisha jitokeza ni pamoja:

Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa, Dkt.  Hussein Ali Mwinyi, Shamsi Vuai Nahodha, Mohammed Jaffar Jumanne, Issa Suleiman Nassor, Prof. Makame Mnyaa Mabarawa na     Haji Rashid Pandu.

Pia wamo:
Jecha Salum Jecha, Dk Dkt. Khalid Salum Mohammed, Rashid Ali Juma, Khamis Mussa Omar, Mmanga Mjengo Mjawiri, Hamad Yussuf Masauni,  Mohammed Aboud, Bakar Rashid Bakari, Hussein Ibrahim Makungu, Ayoub Mohammed Mahmoud na Hashim Salum Hashim


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...