Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman (wa kwanza kulia), akizungumza katika Kikao kifupi na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala B ora walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari Juni 4, 2020, kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, Makamu Mwenyekiti Mohamedi Khamis Hamadi, na kushoto ni watendaji kutoka Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman, akizungumza na ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari Juni 4, 2020,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na watendaji kutoka Wizara yake mara baada ya mazungumzo mafupi kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora,ujumbe huo ulimtebelea ofisini kwake Mjini Unguja Zanzibari Juni 4, 2020.

********************************

Na.Mwandishi Wetu- MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema kuwa Serikali inatakeleza jukumu kubwa la kuwapatia wananchi huduma mbalimbali na kukidhi tafsiri halisi ya utawala bora katika kutekeleza kazi zake.

Akizungumza Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari alipotembelewa na ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amesema kuwa moja ya ishara ya utawala bora katika nchi yeyote duniani ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu kwa sababu ni msingi mkubwa katika kutekeleza majukumu ya Serikali kwa kila mwananchi.

“Haki za binadamu limekuwa ni jambo lenye mjadala kila kona kwa sababu kila jambo linalotendeka liwe zuri au baya ni haki za binadamu, hasahasa jambo likiwa baya utaambiwa umevunja haki za binadamu, Serikali yetu inatimiza jukumu kubwa la kulinda haki za binadamu kwa kila mwananchi na huo ndiyo utawala bora”, Alisema Waziri Suleiman.

Alisema kuwa katika utawala bora Serikali imejenga nidhamu kubwa ya kazi kwa watumishi wote wa umma na imetenga siku ya utawala bora ambayo imeingizwa kwenye siku ya maadili na hapa Serikali inajitathmini kwa mwaka mmoja kipi ambacho imefanikiwa na kipi ambacho hajafanikiwa.

Aidha, Waziri alisema kuwa katika utekelezaji wamasuala ya Utawala bora kwasasa hali ni tofauti na zamani kwani kila mwananchi anapatiwa huduma ya haki kwa kutumia kitengo cha Idara ya Msaada wa Sheria kilichopo Wizara ya Sheria na Katiba ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa kila mwananchi wa Zanzibari.

“Mambo ya utawala bora hapa Zanzibari yalianza zamani wakati wa Rais wa Kwanza wa Zanzibari Hayati Abeid Karume alipoanzisha Wizara ya kuweka hali za wananchi sawa nah ii ilikuwa na madhumi makubwa kwani ilizingatia haki za binadamu kwa upana zaidi”, alisema Waziri Suleiman.

Alibainisha kuwa Tume ina jukumu kubwa la kusimamia haki za binadamu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani kusimamia tafsiri halisi ya neno haki za binadamu, aliongeza kuwa kwenye utawala bora Serikali yetu ya Tanzania umetimiza kwa kiasi kikubwa hasa kuleta maendeleo Makubwa na nidhamu kazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...