Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo wakati akifungua
mkutano wa pili wa kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu
ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza uliofanyika jijini
Dodoma. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi wakuu wa Wizara tano kutoka
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,VIwanda na Biashara, Fedha na
Mipango, Mambo ya Nje ya Nchi, Mifugo na Uvuvi na Kilimo.

Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi),
Dkt. Leonard Chamuriho, akifafanua jambo kwa wataalam (hawapo pichani)
wakati wa kikao cha pili cha kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji
wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza jijini Dodoma.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na Naibu Waziri wa
Kilimo, Omary Mgumba, wakati wa mkutano wa pili wa kujadili namna ya
kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege
cha Mwanza uliofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), Bw. Gilliard Ngewe (kulia), akiteta na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mhandisi Julius
Ndyamukama, wakati wa mkutano wa pili wa kujadili namna ya kurahisisha
usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza
uliofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi,
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Bulayi, akifafanua jambo katika
kikao cha cha pili cha kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa
minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi
(Uchukuzi), Mhandisi Aron Kisaka (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama wakati
walipokutana kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya
samaki kutokea Kwanja cha Ndege cha Mwanza jijini Dodoma.
******************************
Serikali imewaahidi
wafanyabiashara wa minofu ya samaki kuongeza idadi ya mashirika ya ndege
yatakayosafirisha mzigo huo ili kuwafikia walaji kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa jijini
Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack
Kamwelwe, wakati wa kikao cha pili kilichowakutanisha Mawaziri wa Wizara
tano zikiwemo Wizara za Mifugo na Uvuvi, Mambo ya Nje ya Nchi, Viwanda
na Biashara, Fedha na Mipango na Kilimo.
“Mpaka sasa kuna mashirika
zaidi ya mawili ambayo tunafanya mazungumzo nao ili kuleta ndege mkoani
Mwanza, hivyo changamoto zilizojitokeza baada ya kuanza usafirishaji huo
zinaendelea kushughulikiwa’, amesema Mhandisi Kamwelwe.
Waziri Mhandisi Kamwelwe,
amesema baadhi ya changamoto ambazo zimeshashughulikiwa mpaka sasa ni
pamoja na kuanza kwa ujenzi wa uzio na maboresho ya jengo la kutunzia
mizigo.
Aidha, Waziri Mhandisi
Kamwelwe amesema pamoja na jitihada hizo Wizara kupitia kamati
iliyoundwa inaendelea kutafuta masoko ya samaki ili kufikia lengo la
kusafirisha tani zaidi ya 100 kwa safari moja.
Kwa upande wake Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina, amesema pamoja na mzigo wa samaki na
mabondo tayari uzalishaji wa bidhaa za nyama umeanza na wizara
imejipanga kuhakikisha mzigo huo unasafirishwa nje ya nchi ili kuongeza
pato la Taifa na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo mkoani Mwanza.
“Kwa Mkoa wa Mwanza peke yake
uzalishaji wa nyama umeanza na matarajio ni kusafirisha zaidi ya tani
hamsini kwa safari moja, kama Wizara tumejipanga vizuri kwenye jambo
hili na huo ni mwanzo tu”, mesema Mpina.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza,John Mongela ameishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto
zilizojitokeza na kuahidi kuendelea kuhamasisha viwanda kuzalisha zaidi
ili kuongeza pato na kuongeza ajira kwa wanaMwanza.
Katibu Mkuu wa Sekta ya
Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema toka kuanza kwa usafirishaji
huo mapema Aprili 22, mwaka huu, mpaka sasa tani zaidi ya 140
zimeshasafirishiwa ambapo mpango ni kusafirisha zaidi ya tani 100 kwa
safari moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...