Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Shirila la Nyumbu Brigedia Jenerali Hashim Komba (kushoto) wakisaini hati ya
makubaliano kati ya TPA na Shirika la Nyumbu kwa ajili ya kuendelea kutengeneza
terminal treila na kufanya ukarabati wa terminal treila zilizoharibika.Wanaoshuhudia
ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ,Jenerali Venance Mabeyo (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya
TPA Profesa Ignas Rubaratuka na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumbu Balozi
Luteni Jenerali mstaafu Wyjones Kisamba(kushoto).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa
Shirila la Nyumbu Brigedia Jenerali Hashim Komba (kushoto) wakiwa wameshika
hati ya makubaliano ya Nyumbu kuendelea kutengeneza na kukarabati vitendea kazi
vya TPA ikiwemo terminal treila kwa ajili a kubebea makontena.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Venance Mabeyo akizungumza leo jijini Dar es Salaam kabla ya Shirika la Nyumbu
Tanzania kukabidhi terminal treila(tela la kubebea makontena) kwa Mamalaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) .Tela hizo zimetengenezwa na shirika la
Nyumbu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza leo jijini Dar es Salaam
kuhusu uamuzi wa TPA kuamua kutumia Shirika la Nyumbu kwa ajili ya kutengeneza
terminal treila kwa ajili ya kubebea makontena bandarini hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignas Rubaratuka akifafanua wakati wa ghafla ya
ukabidhiwaji wa terminal treila(tela za kubebea makontena) ambayo
yametengenezwa na Shirika la Nyumbu na kisha kukabidhi kwa TPA.
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania(JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali
Venancy Mabeyo wakiwa kwenye tukio la makabidhiano ya treila za kubebea
mankotena yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumbu
Brigedia Jenerali Hashim Komba akitoa ufafanuzi kuhusu terminal treila ambazo
wamezitengeneza na kisha kukabidhi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania(TPA).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali
Venance Mabeyo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) na Shirika la Nyumbu baada ya kufanyika kwa
makabidhiano ya terminal treila.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi wa kada mbalimbali wa TPA na maofisa wa JWTZ.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko(wa pili kulia) akitoa ufafanuzi
kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.
Moja ya Terminal Treila (tela za kubeba
makontena) likiwa katika Bandari ya Dar es Salaam.Treila hilo ni miongoni mwa
treila ambazo zitafanyiwa matengenezo kurudisha kwenye ubora wake na Shirika la
Nyumbu. (PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE).
Said Mwishehe, Michuzi TV
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) pamoja na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kupitia Shirika la Nyumbu wameshirikiana na
kufanikisha mchakato muhimu wa utengenezaji Vichanja (terminal trailers) vya kubebea
mizigo na hasa makontena katika Bandari
ya Dar es Salaam.
Tukio hilo la makabidhiano limefanyika leo Juni
6,2020 na kushuhudiwa na viongozi wa wa TPA, wafanyakazi wa mamlaka hiyo pamoja
na maofisa wa ngazi mbalimbali kutoka JWTZ wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi
Jenerali Venancy Mabeyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi
Mkuu wa TPA Mhandisi Deusidedit Kakoko amesema kukamilika kwa kazi hiyo kunaongeza
kasi ya uvutaji wa makasha na ufanisi wa
kazi za kupakia na kupakua mizigo bandarini. Aidha, ushirikiano huo wa TPA na JWTZ
kupitia Shirika la Nyumbu ni uthibitisho wa utekelezaji wa maelekezo ya
Serikali kwa taasisi zake kujengeana uwezo na kushirikiana katika kuwahudumia wananchi.
"Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
ilingia mkataba na Shirika la Nyumbu linalomilikiwa na Wizara ya ulinzi na
jeshi la Kujenga taifa(JKT)Mei 23,2019.
Mkataba huo uliipatia Nyumbu kandarasi ya kutengeneza vichanja (terminal
trailers) vitano (5) kwa ajili ya Bandari ya Dar es Salaam kwa thamani ya Sh.
524,260,000.
"Katika mkataba huo, Shirika la Nyumbu lilikuwa na majukumu kadhaa ili
kukamilisha utengenezaji wa 'trailers' hizi. Majukumu hayo ni pamoja na usanifu
na utayarishaji wa michoro ya trailers, kufanya tathmini ya upatikanaji wa
malighafi, usanifu na ukataji wa vyuma, kufunga vifaa vya breki na umeme pamoja
kupiga rangi.
"Vichanja (terminal trailers) hizi
zilikabidhiwa kwa TPA Machi 15, na Machi 17, 2020 ukaguzi wa mwisho kwa ajili
ya kukabidhi mradi. Kwa sasa vichanja hivi vipo katika muda wa uangalizi wa
mwaka mmoja. Sote tunajionea kazi nzuri iliyofanyika katika muda mfupi, kwa ubora wa hali ya juu sana na kuokoa kiasi
kikubwa cha fedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza vichanja hivi kutoka nje
ya nchi,"amesema Mhandisi Kakoko.
Ametoa mwito kwa taasisi nyingine za umma na hata
zile za binafsi zinazopata fursa ya kufanya kazi na TPA, kuzingatia gharama
halisi na muda uliowekwa katika kutekeleza kazi zao. "Naomba kutumia fursa
hii kurudia kutoa mwito kwa wateja na wadau wa sekta ya bandari kuendelea kuzitumia
bandari zetu kote nchini sambamba na kuitunza miundombinu yake kwa faida ya
sasa na siku zijazo".
Kwa
upande wake MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amesema anatoa shukrani kwa uongozi wa Shirika la Nyumbu na TPA kwa kupata fursa ya
kushuhudia makabidhiano ya vifaa hivyo ambavyo vimetengenezwa na
Nyumbu."Ni tukio la kihistoria taasisi moja kufanya kazi na taasisi nyingine,
kumekuwa na tabia ambayo imejengeka kuwa muda mrefu wa kuamini
vinavyotengenezwa nje ni bora zaidi kuliko vinavyotengenezwa hapa hapa nchini.
"Natoa shukrani kwa uongozi wa bandari kwa
kutuamini na kutupa kazi ya kutengeneza vichanja hivi na tunajisikia fahari
tunaposhirikishwa kujenga uchumi wa nchi
kwa kushirikiana na taasisi nyingine. Jeshi la Wananchi wa Tanzania linaonesha
namna ambavyo linaweza kufanya mambo mengi , kuna vijana wengi wasomi na watalaam
walioko jeshini ambao wanao uwezo mkubwa wa kufanya mambo makuwa,"amesema.
Jenerali Mabeyo amesema kuwa fursa ambayo
wameipata ni changamoto ya kuongeza jitihada katka utendaji kazi wao wa kila siku, huku akitumia nafasi hiyo kueleza
kuwa watalimarisha shirika la Nyumbu ikiwa ni pamoja na kuongeza
askari."Nyumbu lilikuwa ni shirika la utafiti lakini sasa tunafanya tafiti
na kisha tunazalisha. tunashukuru TPA kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata
wakati wote."
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya TPA Profesa Ignas Rubaratuka amesema kwa kipekee wanamshukuru Mkuu wa Majeshi kwa kutenga muda wake na kushuhudia makabidhiano hayo ya kazi nzuri
iliyofanywa na vijana wazalendo ambao wamethibitisha kuwa pamoja na weledi
uliotukuka katika shughuli za ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini pia Jeshi
letu ni kiungo muhimu katika kazi za fani mbalimbali zenye mchango mkubwa
katika Ujenzi wa Taifa letu.
"Jumuia nzima ya TPA tumefurahishwa sana tukio hili
na ubora wa Vichanja hivi. Kazi hii imefanyika kwa muda mfupi, kwa kutumia waataalamu
wa ndani ya nchi yetu na gharama nafuu ambazo ni halisi. Hakika, ushirikiano
huu ni ushahidi kuwa, taasisi za umma zikiamua kushikana mkono na kuwezeshana,
matokeo yake huwezesha kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa kwa wakati.
Pia amesema kazi nzuri iliyofanywa na Shirika la Nyumbu , TPA imeamua
kusaini Mkataba wa ushirikiano (MoU) wa kipindi cha miaka
mitatu(03) ili Jeshi letu Kikosi cha Nyumbu wafanye kazi nyingine ya
kutengeneza Vichanja vipya na kukarabati vichanja chakavu vinavyotumika Bandarini.
"Tunaamini kuwa, kupitia ushirikiano huu na
uwezo mkubwa wa Jeshi letu,kazi hii itafanyika kwa kuzingatia ubora, gharama
nafuu na halisi. Tunawatakia kila jema katika kutekeleza kazi hii,"amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...