Na Mwandishi wetu, Pretoria
Kundi la pili la Watanzania waliokwama nchini Afrika Kusini kutokana na Lockdown nchini humo iliyosababishwa na ugonjwa wa Corona linatarajia kurejeshwa nchini mwanzoni mwa wiki ijayo mara tu baada ya taratibu za safari hiyo kukamilika, imefahamika.
Kwa mujibu wa ubalozi wa Tanzania nchini humo, jumla ya Watanzania 63 wamekuwa katika harakati za kutaka kurejea nyumbani lakini wamekwama kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuchelewa kwa vibali vya kusafiri nje ya nchi hiyo kwa mujibu wa sheria za huko.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst.) Gaudence Milanzi amekutana na kufanya kikao na Watanzania hao ubalozini jijini Pretoria leo na amewaomba wawe na subira na kuwaahidi kufanya kila liwezekanalo kutatua changamoto wanazokabiliana nazo.
Changamoto walizomueleza Balozi ni pamoja na kuishiwa fedha za kuishi nchini humo, ambapo wengine wakitarajia kuondoka walikuwa tayari wamerudisha nyumba walizokuwa wakiishi na kulazimika kulala nje, kadhalika kuchelewa kwa mabasi ya kuwachukua pamoja na kutopatikana kwa haraka vibali vya kuwaruhusu waondoke kumechangia.
Katika kikao hicho, Balozi Milanzi aliwahakikishia Watanzania hao kwamba ubalozi unahaha usiku na mchana kutafuta ufumbuzi wa changamoto walizonazo, na kwamba upo karibu na uongozi wa umoja wa Watanzania waishio nchini humo ambao amesema umekuwa ukitoa ushirikiano wa kutosha.
Balozi Milanzi aliwaelezea juu ya utaratibu wa vibali ulivyo na utaratibu wa serikali husika huku akiwahakikishia kwamba ubalozi unajua matatizo yao na tayari vibali hivyo vilikwisha ombwa na vinasubiriwa kutoka serikali za Zimbabwe, Zambia na Afrika Kusini.
Balozi aliwaeleza kuwa changamoto zao zote anazifahamu na wasione kuwa hana habari, hivyo wakiona Afisa ubalozi anashughukika wajue kwamba amemtuma kufanyia kazi changamoto walizonazo.
Endapo kama vibali vitapatikana Jumatatu ama Jumanne kama inavyotarajiwa, Watanzania hao wanatarajiwa kuondoka hiyo Jumanne au Jumatano ya wiki ijayo kwa njia ya barabara.
Kundi la kwanza la Watanzania waliokwama Afrika Kusini lilirejea nyumbani Jumatatu Mei 25, 2020 ikiwa ni pamoja na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama kutokana na Lockdown na kusitishwa safari za ndege inayoendelea huko, kutoka Johannesburg kuja Dar es salaam.
Jumla ya Watanzania 14 ambao walikwama nchini humo kwa miezi miwili kufuatia Lockdown hiyo pamoja na raia 12 wa Afrika Kusini pamoja na raia mmjoa wa Uingereza nao wakajiunga kwenya msafara huo baada ya kuona ni afadhali warejee Tanzania ambako hakuna Lockdown ili kuendelea kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo.
Akiwasindikiza abiria hao wa kundi la kwanza walioondoka kwa ndege ya kukodi ya kampuni ya AS SALAAM AIR ya Zanzibar, Balozi Milanzi aliwapa pole kwa kuwa katika Lockdown ya miezi miwili na kuwatakia safari njema na maisha ya furaha watapowasili Tanzania ambayo ni nchi pekee ambayo imekuwa na msimamo thabiti wa kupambana na gonjwa la COVID 19 bila kufungua mtu ndani.
Sehemu ya Watanzania waliokwama Afrika Kusini wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst.) Gaudence Milanzi (kushoto) alipoongea nao Ubalozini jijini Pretoria leo
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst.) Gaudence Milanzi akiwa katika kikao na Watanzania hao waliokwama Afrika Kusini
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst.) Gaudence Milanzi akiwa katika mazungumzo na Watanzania hao .
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst.) Gaudence Milanzi (katikati) akiwa na Watanzania hao baada ya kikao ubalozini
Watanzania hao wakipata chakula baada ya kikao na Balozi Milanzi Ubalozini Pretoria

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...