
Yassir Simba,
Michuzi Tv
Sakata la mchezaji
wa Young Africans raia wa Ghana,Bernard Morrison limechukua sura mpya ambapo
kupitia nakala iliyotolewa na kaimu katibu mkuu wa klabu ya Yanga Wakili Simon
Patrick leo tarehe 24/06/2020 klabu ya
Yanga imeamua kumkata kiasi cha shillingi 1,500,000 pesa taslimu ya
kitanzania mchezaji huyo kutokana na
kile kinachdaiwa na klabu hiyo kuwa mchezaji huyo alifanya mahojiano na chombo
cha habari bila kufuata utaratibu uliowekwa na kabu.
Katika siku hizi za
hivi karibuni kumekuwa na malalamiko juu ya mkataba ya mchezaji huyo kwa kile
kinachodaiwa kuwa kuna baadhi ya timu zinatajwa kumnyemelea mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 27,ikumbukwe Yanga na Morrison waliingia mkataba wa miezi
saba na mchezaji huyo kuanzia tarehe 15/01/2020
mpaka 14/07/2020 kwa kuwa na makubaliano na mchezaji kuwa endapo klabu
itaridhisha na kiwango chake mkataba utaongezwa ambapo mara baada ya Yanga
kuridhishwa na kiwango chake tarehe 20/03/2020 klabu hiyo ya Yanga iliingia
mkataba na Morrison kwa kuzingatia maslahi binafsi ya mchezaji huyo ambapo
mkataba huo uliotakiwa kumalizika 14/07/2022 .
Mara baada ya Yanga
kumuongeza mkataba mchezaji huyo, klabu hiyo iliusajili mkataba huo kwenye
mifumo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na shirikisho la Mpira wa
MIguu Duniani ( FIFA)
Katika siku za
nyuma Morisson aliwahi kugomea kujiunga na timu katika michezo ya ligi kuu ya
Tanzania bara ikiwemo mchezo wa Yanga dhidi Mwadui pamoja na Yanga dhidi ya JKT
Tanzania ambapo Benard Morrison hakujiunga na timu licha ya kufanya mazoezi na
timu pamoja na jina lake kujumuisha katika kikosi cha wachezaji watakao safiri
na timu
Kupitia nakala
iliyotolewa na klabu imesisitiza kuwa endapo kuna klabu yoyote inayomtaka mchezaji
huyo benard MOrrison ifuate sheria na taratibu zote kwa maana Morrisn bado ni
mchezaji halali wa Yanga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...