Tunaomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika Jukwaa la kipekee na la ya aina yake Stara Fashion Week, litakalofanyika tarehe  24th na 25th July 2020 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Sanaa Ya Taifa Posta  Opp IFM.

Jukwaa hili linafanyika kwa Mara Ya Sita Mwaka huu na litajumuisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka kila kona ya Tanzania  Fashion show itaanza saa 10Jioni hadi saa 12 jioni na kusindikizwa na Tuzo na burudani za kila aina. Kauli mbiu ya Stara Fashion Week 2020 ni ubunifu wenye tija,  Eco Fashion.

 Jukwaa hili Mwaka huu linawaleta pamoja wabunifu katika harakati za kutunza Mazingira katika industry ambayo inatajwa kuwa ya pili katika uchafuzi wa Mazingira Duniani.

Jukwaa hili si tu linataka kuongeza ufanisi kwa Wabunifu shiriki lakini pia kuwataka wabunifu hao kuchukua hatua na  kuhamasisha jamii katika suala la Mazingira na Mavazi. 

Kwa njia hii si tu  Wabunifu wanaweza kulinda na kutunza Mazingira bali pia wanaweza kujiongezea kipato kupitia mabaki wanayozalisha na kuyatupa yenye wastani wa takribani gunia mbili kwa wiki.

Wabunifu hawa wamepitia semina elekezi ya namna ya kupunguza Taka (Reduce), kubadili matumizi (recycle) na kutumia upya (Reuse) na wako tayari kuwa mfano wa wabunifu Wanaojali  Kulinda na Kutunza Mazingira. Mkakati huu ni kelele za "wito wa kutaka hatua zichukuliwe.” Utunzaji wa Mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu.

Pamoja na jukwaa hili Mnakaribishwa kufanya manunuzi mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali na wafanyabiashara  katika maonyesho ya biashara yatakayoanza asubuhi mpaka saa 12 jioni. NIBUREE HAKUNA KIINGILIO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...