Asisitiza watu kukataa kupokea barakoa wasizojua zinatoka wapi...
 
Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

RAIS Dk.John Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa Watanzania wasikubali kupewa msaada wa barakoa na kisha kuzivaa bila kujua zilikotoka kwani hiyo huenda ikawa njia nyingine ya kuingiza Corona nchini.

Amefafanua licha ya kutoa maelekezo na maagizo kwa Wizara ya Afya na kwa viongozi wa mikoa na wilaya ameshudia watu wakipewa barakoa na juzi kwenye taarifa ya habari ameona kuna grupu linajiita Magufuli Forum likagawa barakoa na wala halijui limetoka wapi ingawa hashangai mtu akijiita Magufuli au hata akijiita Fisi.

Akizungumza leo mbele ya mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Rais Magufuli pamoja na kueleza mambo mbalimbali ambayo yamefanywa na Serikali ametumia nafasi hiyo kusisitiza kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona hata kama ugonjwa umepungua kwa kiasi kikubwa.Wakati anazunguzia barakoa Rais Magufuli alisema kuwa "Ingawa siku nyingine Spika akiwa bungeni kwenye kiti chake peke yake alikuwa amelivaa libarakoa mdomoni.

"Ndugu zangu Watanzania tumtangulize Mungu na nitoe mwito kwa viongozi mbalimbali kwasababu njia nyingine inayoweza kutumika ni ya kuletewa vifaa vya Corona vyenye corona,"amesema Rais Magufuli.

Ameongeza watu watakuja kuwaambia vaeni barakoa."Mtu anapokuletea barakoa hujui hata ameitoa wapi kataa mwambie akavae yeye na mkewe na watoto wake nyumbani.

"Tutaumizwa jana , juzi nilikuwa nasikiliza kwenye taarifa ya habari kuna grupu moja linaitwa Magufuli Forum , wala mimi silijui.Mtu kujiita Magufuli au hata akijiita Fisi ni yeye mwenyewe lakini walikuwa wanagawa barakoa wala hazijulikani zinatoka wapi wakati nilishatoa maelekezo kwa Wizara ya afya na kwa viongozi wa mikoano na wilayani.

"Ukimuona mtu anagawa barakoa kwa wananchi ashikwe akaulizwe zimethibitisha na wizara ya afya au zimethibitishwa na nan.Tutaumia kwa kukosa maarifa, ukitaka kuvaa barakoa kashone yako. Mbona ni rahisi tu barakoa imekaa kama titi la mtu mmoja limekatwa upande mmoja, weka huku kamba, walimu hoyee,"amesema.

Ameongeza kuwa "Hapo nilikuwa nachomekea tu kidogo lakini ninachotaka kusema kila mtanzania, tuko milioni 60 kila mmoja achukue tahadhari, tusidanganywe kwa kuletewa mabarakoa ambayo hatuji yametoka wapi , tukaletewa Corona bila sisi kujua.

"Ugonjwa huu umepungua na nina uhikika utaisha kwasababu Mungu yuko pamoja na sisi , tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu kwa hiyo ndugu zangu walimu katoeni elimu hiyo tutashinda na ndio maana mmeona ndege zimeanza kuja , na ndio maana mnaona sisi hatukuweka Lockdown.

"Ukiweka Lockdown maana yake hakuna kitu kingekuwa kinafanyika, miradi yote hii ingekuwa imesimama, watu wasingeenda mashambani , huwezi kwenda kulima mahindi yako, huwezi kwenda kuvuna mpunga wako, ukishajilock down umejiua.

"Lakini tukaambiwa tuweke lock down tusiende Kanisani na Msikini ile ni kufuru watu kwenye shida walimkimbilia Mungu, sisi tunakimbilia ndani .Tulitaka kumpa utawala shetani badala ya kumeweka Mungu aliyetuweka duniani,"amesisitiza Rais Magufuli na kuongeza Tanzania tumeshinda vita dhidi ya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...