Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) Mkoani Manyara inamshikilia
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Maisaka kati Bakari
Khatibu na katibu wa Tawi hilo Juma Swalehe wote wakazi wa wilaya ya
Babati kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya sh. 200,000 kutoka kwa
Mwinjilist wa kanisa la kinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) mtaa wa
Komoto.
Mkuu wa Takukuru Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu aliyasema hayo mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Makungu
alisema viongozi hao waliomba rushwa ya sh. 200,000 kinyume na kifungu
15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Alisema
wawili hao waliomba na kupokea fedha hizo kutoka kwa Mwinjilist wa
kanisa la KKKT Komoto kwa maelelezo kuwa baada ya kupokea fedha hizo
wangemwachia kiwanja walichokuwa wakidai kuwa ni mali ya CCM.
Alisema
kuwa uchunguzi zaidi kuhusiana na uhalali wa CCM kumiliki kiwanja hicho
na Mamlaka ya viongozi hao kuhusiana na mali za chama unaendelea na
mara utakapokamilika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
"Rai
yetu kwa viongozi wachache ndani ya chama tawala hasa wa ngazi za chini
wenye utajiri wa fikra haba wanaopitapita wakiwaaminisha wananchi kuwa
hawawezi kuguswa na Takukuru kwa kua chama kilichowaajiri ndicho
kinaongoza serikali," alisema Makungu.
Aliwakumbusha
viongozi wa aina hiyo ibara ya 13(1) (5) ya katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania na kunuu" Watu wote ni sawa mbele ya sheria na
wanayo haki bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria bila kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni
yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali ya maisha,"Alisisitiza
Alisema
kwa msingi huo katiba uwe wa chama tawala au vyama vingine vya
upinzani, sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007
inakuhusu ili mradi nafasi yako iwe ni kutelekeza majukumu
yanayohusiana na umma wa watanzania hivyo watendaji ndani ya chama
tawala ni vyema pia wakafahamu kuwa hawako juu ya sheria na anayekiuka
hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake kama ilivyo kwa watu wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...