Charles James, Michuzi TV

KAMISHNA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk Mussa Juma amesema mamlaka hiyo inatarajia kutoa Sh Bilioni 2 ikiwa ni mchango wake kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Dk Juma amesema hatua hiyo inakuja baada ya sekta hiyo ya Bima kukua nchini na hivyo kuonelea kwamba inawapasa nao kama mamlaka kuchangia mfuko huo.

Hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akijibu maswali na hoja za wabunge ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti ambayo ilikutana na mamlaka hiyo bungeni na kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusiana na ukuaji wa mamlaka hiyo.

Amesema TIRA imekua ikitekeleza sheria inayowataka kutoa asilimia 15 ya mapato yao kwenye mfuko mkuu wa serikali na wamekua wakifanya hivyo ambapo ndani ya kipindi cha miaka mitatu michango yao imekua ikiongezeka kila mwaka.

"  Tumekua tukitekeleza sheria hiyo inayotutaka tutoe asilimia 15 na kwa mwaka 2016/17 Mamlaka ilitoa mchango wa Sh Bilioni 1.86, mwaka 2017/18 tulitoa Sh Bilioni 1.79 na mwaka 2018/19 tulifanikiwa kutoa Sh Bilioni 1.99 na kwa mwaka sasa tunatarajia kutoa zaidi ya Bilioni mbili.

Niseme tu TIRA tunayo mikakati kabambe na mikubwa ya kufanya maboresho ya kimfumo na ambapo tunaamini mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu tutakua tunatoa huduma za bima kwa mfumo wa kielektroniki," Amesema Dk Juma.

Kwa upande wake Meneja wa TIRA Kanda ya Kati, Stella Rutaguza amesema ingawa sheria hailazimishi mfanyabiashara kukatia Bima mizigo inayoagizwa nje ya Nchi lakini pindi atakapoamua kukata basi anatakiwa kutumia Kampuni za Bima za ndani ya nchi.
 MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti, Mashimba Ndaki, akito mchango wakati Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA) wakitoa elimu ya Bima kwa Kamati hiyo
 KAMISHNA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania (TIRA), Dk. Mussa Juma akitoa elimu ya Bima kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...