MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tundu Lissu
 
 
Na Said Mwishehe, Michuzi TV


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi Tundu Lissu ametangaza rasmi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka 2020.

Lissu ambaye amekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu kwa nyakati tofauti amekuwa akionesha nia ya kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hatimaye leo ametangza rasmi nia hiyo kwa kueleza kuwa anayo nia thabiti ya kuwatumikia Watanzania.

Akitangaza nia yake hiyo leo Juni 8, 2020 kupitia mitandao ya kijamii, Lissu amesema kama ambavyo imekuwa jadi ya nchi yetu, Jumapili ya mwisho wa Oktoba 25 kila baada ya miaka tano Watanzania hupiga kura ili kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali kwa ngazi ya udiwani, ubunge na urais.

"Sasa kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu na itakapofika Oktoba 25 ya mwaka huu ambayo itakuwa siku ya Jumapili sisi wananchi katika wingi wetu tutafurika kwenye vituo vya kupiga kura katika sehemu mbalimbali za nchi yetu kwa ajili ya kuchagua viongozi,"amesema Lissu.

Amesisitiza kuwa kama amewahi kueleza huko nyuma ya kwamba atagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo hii ameamua kuitangaza rasmi kuwa atagombea nafasi hiyo ya juu katika nchi yetu.

"Nataka kuutangazia umma wa Watanznia kokote waliko, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi, mwaka huu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ,nagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,"amesema Lissu.

Amefafanua tayari amewasilisha taarifa rasmi ya nia hiyo kwa katibu Mkuu wa Chama chake(CHADEMA)kama ilivyoelekezwa kwenye utaratibu ulitolewa na Chama hicho."Ninawajibu wa kutaja kile ambacho kimenisukuma kupataka kugombea nafasi hii ya juu kabisa kwenye mfumo wa uongozi katika nchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu .

"Pamoja na mambo mengine mengi yalinisukuma kugombea nafasi hii ya urais, ukweli nataka kuwatumikia Watanzania kwani ninazo sifa zote na hakuna kipingamizi cha aina yoyote cha kunizuia kugombea urais au nafasi nyingine yoyote ya uongozi,"amesema Lissu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...