Ujenzi wa eneo la lango (Water Intake) la kuingilia maji kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme katika Mradi wa Julius Nyerere (Mw 2115) unatarajiwa kukamilika Februari 2022.

Mhandisi Dismas Mbote, Mhandisi wa ujenzi njia za maji pamoja na Bwawa kwenye Mradi wa Julius Nyerere amesema utekelezaji wa njia hiyo ulianza Mwezi Oktoba 2019.

Aliongeza kuwa kazi ya uchimbaji wa lango imekamilika kwa kuchimbwa kina cha mita 53 ambapo hivi sasa kazi inayoendelea ni uondoaji wa kifusi na uchimbaji wa mahandaki matatu yatakayotumika kupitisha maji.

"Vifusi ambavyo vinachimbwa katika mradi huu wa Julius Nyerere havitupwi, mawe yanasagwa na kuwa mchanga, kokoto na mawe mbalimbali ambayo hutumika kwenye ujenzi", alisema Mhandisi Mbote.

Aidha, zitafanyika kazi za kuchoronga miamba pamoja na kuimarisha kuta kwa zege.

Maji yatakayo fua umeme kabla ya kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yataingia kwanza kwenye lango.

Pia kwa hivi sasa imeletwa mashine ya kuchoronga miamba ambayo ni ya kwanza kwa Tanzania na inayotarajiwa kuongeza kasi katika uchimbaji wa mahandaki ya kupeleka maji kwenye mitambo. 

Handaki la kwanza litakuwa na urefu wa mita 350, la pili mita 410 na la tano mita 570 hadi kwenye mitambo ya kufua umeme.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...