Mkurugenzi wa Cornwell Tanzania Naturopath (wa pili kulia) Elizabeth Lema akioesha moja ya dawa asili ambayo ilikuwa ya kwanza kuisajali baada ya Rais Dk.John Magufuli kuingia madarakani ambapo ametumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna inavyowajali na kuwapa kipaumbele.Wengine kuanzia  kushoto ni Meneja Juma Meneja, Mkurugenzi Johanny Brinkman na kulia ni Dk. Ralph Brinkman.
Elizabeth Lema ambaye ni Mkurugenzi wa Cornwell Tanzania Naturopath( wa pili kulia) akionesha moja ya cheti ambacho wamepewa na mamalaka zinazohusika na mamlaka za Serikali ikiwemo ya Wizara ya Afya kwa ajili ya kuendelea na utoaji huduma.Kulia ni Dk. Ralph Brinkman na wa kwanza kushoto ni Meneja Pili Juma, Mkurugenzi Johanny Brinkman.
Mkurugenzi wa Cornewell Tanzania Naturopath Clinic (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 7,2020 kuhusu Clinic hiyo ambayo imekuwa ikijihusisha na utoaji matibabu kwa njia ya tiba asili na tiba mbadala.Wengine ni watumishi wa Clinic hiyo.
Mkurugenzi wa Cornewell Tanzania Naturopath Clinic (kushoto) na Dk. Dk. Ralph Brinkmann ambaye ni daktari wa clinic hiyo wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Juni 7 mwaka 2020.
Watumishi wa Cornewell Tanzania Naturopath Clinic kuanzia kushoto ni Meneja Pili Juma, Mkurugenzi Johanny Brinkmann, Mkurugenzi Elizabeth Lema pamoja na Dk. Ralph Brinkmann wakiwa kwenye picha ya pamoja leo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu clinic hiyo.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UONGOZI wa Clinic ya Cornewell Tanzania Naturopath umetoa ombi kwa Serikali kuendelea kufanya maboresho ya sheria inayohusu tiba mbadala na asili ili kuendana na mazingira yaliyopo hapa nchini huku ukitumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Tano.

Akizungumza leo Juni 7 mwaka 2020, Mkurugenzi Mwanzilishi wa Clinic ya Kimataifa ya Cornwell Tanzania Elizabeth Lema amesema moja ya changamoto ambayo walikutana nayo wakati wanaanza ilikuwa ni sheria lakini wanashukuru kwa sasa hali imekuwa nzuri na kuendelea kutoa ombi kwa wanaohusika na tiba asili na tiba mbadala kuboresha zaidi.

Amesisitiza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli kwa kulipa wepesi suala hilo na kuwezesha baadhi wawekezaji kusajili biashara zao hususani zinazohusika na Tiba za asili na mbadala kuweza kusajiliwa. "Kitendo cha Rais Magufuli kuingia madarakani kimewezesha tiba mbadala na Tiba asili kupata usajili ingawa Sheria haibadishwi kwa siku moja,"amesema Lema.

Pia amesema kuwa kutokuwa na elimu ya sahihi ya tiba mbadala na asili baadhi ya watendaji wa Serikali ilikuwa kikwazo kwao katika kupata vibali na upatikanaji usajili kwa muda muafaka.Ipo haja ya Serikali kuangalia viwango vya dawa vinavyolingana na mazingira ya nchi yetu tofauti na hivi sasa ambapo vinaangaliwa."

Wakati huo huo Dk.Johnn Brinkmann ameongeza kwa sababu ya umuhimu wa dawa hizo nchini Cornwell Tanzania wameamua kuanzisha Chuo kitaachokuwa kinatoa mafunzo ya tiba asili na mbadala na hiyo ni kwa sababu ya kukosekana chuo chenye mafunzo hayo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

"Katika chuo chetu kutakuwa na kozi mbalimbali za muda mfupi ngazi ya astashahada na stashahada na elimu kwa mtu binafsi anayetaka kufahamu masuala ya tiba mbadala au kuangalia Afya yake,"amesisitiza. Pia amesema kuwa sababu nyingine ya kuanzisha chuo hicho ni kwa sababu Tanzania ina miti dawa nyingi ambayo inahitaji kuendelea kufanyiwa Utafiti na kutimika katika Tina.

Katika hatua nyingine amesema kuanzia kesho Clinic hiyo itaanza kutoa huduma ya vipimo vya afya bure ili waweze kujua afya zao na kupatiwa matibabu."Tutatoa vipimo bure na kawaida kipimo hiki gharama yake kwa bei ya kawaida ni Sh.70,000 lakini tumeamua ndani ya mwezi mmoja kuanzia kesho tutatoa bure.

Daktari wa kituo hicho Ralph Brinkmann ameshauri kutokana na mfumo wa vipimo unaotumika Ni vyema watu wenye umri wa kuanzia miaka 8 na kuendelea kupata Huduma hiyo.

"Kipimo hiki ambacho tutaanza kukitoa kwa wananchi watakaofika kwenye Clinic yetu tutapenda zaidi wenye kuja kupima wawe na umri kuanzia miaka nane na kuendelea lakini chini ya umri ya miaka nane itakuwa ngumu kutokana na majibu sahihi,"amesema.

Hata hivyo umesema katika Clinic hiyo wanatoa huduma ya matibabu mbalimbali kwa wanaokwenda kupata huduma.Baadhi ya magonjwa ambayo wanatibu ni sukari, figo, magonjwa ya moyo na magonjwa mengine sugu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...