Na Said Mwishehe,Michuzi TV
WAENDESHA wa usafiri Bodaboda wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wametakiwa kufuata sheria katika kutoa huduma hiyo ya kubeba na kusafirisha abiria kutoka eneo moja kwenda jingine.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema hayo wakati akizungumza na Michuzi Blog, ambapo amefafanua kuwa kuna kila sababu ya kuhakikisha waendesha bodaboda wanazingatia sheria kwani wale ambao watabainika kukiuka watachukuliwa hatua.
Hata hivyo amesema kwa sasa hali ya usalama ni kubwa zaidi ndani ya Wilaya hiyo na hata matukio ya watu kuporwa bodaboda yamepungua."Hali ni nzuri sana kwasababu hata matukio makubwa yaliyokuwa yanatokea huko nyuma kwa saa hayapo tena".
Ametumia nafasi hiyo pia kuwaonya waendesha bodaboda ambao wanatumia usafiri huo kufanya matukio ya uhalifu na kuacha shughuli za kusafirisha abiria. "Waendesha bodaboda ambao nao wanakwapua waache kufanya hivyo mara moja.Tuwakamata na kuwachukulia hatua".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...