***************************
NA MWAMVUA MWINYI 

WAJASIRIAMALI wa Kikundi cha Mwanzo Mgumu, kilichopo Kijiji cha Kwedikwazu Kata ya Kabuku wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, wanahitaji usafiri utaowarahisishia kazi zao za ubebaji wa mawe. 

Wakizungumza na Waandishi wa habari katika eneo wanalofanya shughuli zao za kubangua mawe, Wajasiriamali hao walisema kuwa wananufaika na machimbo ya mawe yanayotumika kutengenea Marumaru na Jipsam katika majengo mbalimbali. 

Katibu wa kikundi hicho Saumu Kisaka alisema kuwa wananunua mawe kutoka katika Makampuni yanayochimba mawe Kijijini hapo, wananunua plastiki moja shilingi elfu 2,000 wanayabangua kisha wanauza kwa shilingi 3,000, hivyo wanapata pesa za kujikimu na familia zao. 

Asia Omary Mjumbe alisema kuwa kikindi chao kilikopa shilingi milioni 5 kutoka Halmashauri ya Handeni, ambazo wanataraji kuumaliza wakati wowote, na kwamba wanataraji kukopa pesa zaidi kwa ajili ya kukiendeleza biashara yao. 

“Tunakutana kila wiki ambapo kila mwanachama anachangia shilingi 5,000 mpaka sasa tuna kiasi cha shilingi milioni 2 benki, lakini moja ya changamoto nyingine tunayokabiliana nayo ni ubanguaji wa mawe haya kwa mikono,” alisema. Kibibi alisema kuwa wakimaliza mkopo wa Halmashauri wanataraji kuomba mkopo wa milioni kumi, lakini kiu yao ni kumiliki gari ndogo watahoitumia kubeba mawe kutoka katika machimbo yaliyopo kijijini hapo. 

Nae Mwenyekiti wa Mwanzo Mgumu Zaina Mwelugala aliishukuru Serikali chini ya rais Dkt. John Magufuli kwa juhudi kuhimiza viwanda, kwani nao wananufaika kupitia wawekezaji waliopo ikiwemo wao kununua mawe, kuyagonga kisha kuuza kokoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...