HATIMAYE Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kondoa limekamilisha rasmi kikao cha kawaida cha robo ya nne baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano tangu lilipoingia madarakani mwezi Oktoba 2015 na kufanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka  shilingi milioni 400 kwa mwaka 2016/2017 hadi kufikia shilingi bilioni 1.6 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la zaidi ya  asilimia 135.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa, Msoleni Dakawa katika kikao  cha  kawaida cha kuvunja Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.

“Kuongezeka kwa mapato kumetokana na usimamizi mzuri wa Waheshimiwa Madiwani katika matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato wa Serikali za Mitaa unaotumia mashine za kukusanyia mapato “POS”,alisema Mkurugenzi Dakawa.

Aidha  katika upande wa rasilimali fedha Mkurugenzi amesema kuwa Halmashauri imeendelea kufanya vizuri katika usimamizi wa matumizi ya fedha na ufungaji wa hesabu kulikopelekea kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo  kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

“ Uongozi ni dhamana na kipimo cha utumishi ni jinsi ambavyo tunaweza kusimamia utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo, hivyo nawaomba watumishi wote kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana katika kusimamia maendeleo na kuibua vyanzo vipya vya mapato,pia ninaawashukuru sana Waheshimiwa Madiwani kwa utendaji kazi wenu mzuri toka mwanzo hadi mwisho mmefanya  kazi kubwa ya kuleta maendelao  kwa Halmashauri yetu kwa uzalendo na uvumilivu,” alisisitiza Mkurugenzi  Dakawa.

Akielezea mikakati iliyowekwa na Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato alisema kuwa Halmashauri imewekeza katika miradi mkakati itakayotumika kama vyanzo vya mapato kama vile ujenzi wa stendi ya mabasi na Malori Bicha, ujenzi wa machinjio Bicha pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Aidha Mwenyekiti waHalmashauri ya Mji Kondoa Mhe. Hamza Mafita alimshukuru  Mkuu wa Wilaya Mhe. Sezaria Makota, Mkurugenzi, Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa Chama pamoja na wakuu wa Idara kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wote wa uongozi wake.

“Tuliamua fedha za TARURA zijenge barabara mjini  kwa kiwango cha lami kila mwaka angalau kilomita moja na nusu, pia tumeomba tuongezewe  mifereji na taa za  Barabarani.Hali kadhalika tumejitahidi kupunguza kero ya maji kwa wananchi kwa kuleta mashine mbili ambazo zitasaidia upatikanaji wa maji kwa wingi  kikubwa zaidi najivunia Uongozi wangu hatujawahi kupata hati chafu  hii yote inamaanisha tumesimama imara.

Baraza la Waheshmiwa Madiwani Halmashauri ya Kondoa mji limehairishwa rasmi  ambapo mgeni rasmi katika  baraza hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe Sezaria Makota  na kuhudhuriwa na  Waheshimwa madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wananchi.
 Baraza la Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota (wa pili kutoka kulia waliokaa) wakati wa baraza la mwisho la waheshimiwa madiwani kilichofanyika hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Makota (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa madiwani wanawake.
 Wananchi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliojitokeza kufuatilia Baraza la mwisho la waheshimiwa madiwani katika ukumbi wa Kondoa Irangi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...