Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama
Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo
Juni 21 ,2020 jijini Dar es Salaam kuhusu tamko lao kuelekea uchaguzi Mkuu
unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia ni Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo
John Mlabu.
Kulia ni Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo John
Mlabu(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama
Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(kulia) akimkaribisha rasmi kada wa Chadema
Tundu Lissu kwenye jumuiya ya walemavu huku akitumia nafasi hiyo kumtaka
kuungana nao katika uchaguzi mkuu mwaka huu kwa kumchagua Rais Dk.John Magufuli
ili waendelee kunufaika na mambo mazuri yanayofanywa na Dk.Magufuli.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kutoka Chama
Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(aliyevaa kofia nyeusi)akiwa na wajumbe wengine
wa jumuiya hiyo wakiangalia sehemu ya hotuba ya Mwenyekiti huyo baada ya
kumalizika kwa mkutano kati yao na waandishi wa habari.
Wajumbe wa jumuiya hiyo ya CCM ya Watu wenye
ulemavu Charles Temba(kushoto) na Lameck Samson wakifuatilia kwa makini mkutano
huo.
Mjumbe wa jumuiya hiyo Hamza Waritu akiwa makini
kusikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu CCM wakati akizungumza
na waandishi wahabari leo Juni 21,2020 jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wajumbe wa jumuiya hiyo Ashura Narino
akifuatilia mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama
Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(kushoto), Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo John
Mlabu(katikati) na Mjumbe wa jumuiya hiyo Charles Temba wakiwa makini
kusikiliza maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano
huo uliofanyika leo Juni 21,2020 jijini Dar es Salaam.
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
JUMUIYA ya Walemavu wa Chama Cha kupitia Chama Cha
Mapinduzi(CCM) wamemkaribisha rasmi Kada wa Chadema Tundu Lissu kujiunga na
jumuiya hiyo baada ya kupata ulemavu huku wakitoa msimamo kuwa katika Uchaguzi
Mkuu mwaka huu walemavu wote kura kwa Rais Dk.John Magufuli.
Akizungumza leo Juni 21,2020 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Walemavu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) Peter Sarungi ameeleza
wazi walemavu wote wanatakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuhakikisha
anashinda na kwenye nafasi hiyo ya urais hakuna mtu mwenye ulemavu atajitokeza
kumpinga Rais Magufuli zaidi ya kumpigia kura ya ndio.
Akifafanua zaidi kuhusu Lissu ambaye wamesikia ni miongoni mwa
wanaotaka kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadma, kwanza wanamkaribisha
rasmi kwenye jumuiya ya watu wenye ulamavu kwasababu uumbaji wa Mungu
haujamalizika mpaka mtu aingie kaburini na ndio maana kuna msemo usemao hujafa
hujaumbika.
"Kipindi cha nyuma tunajua Lissu hakuwa mtu mwenye ulamavu
,ameupatia ukubwani na hatujui kaupataje pate, na tunajua siasa
zake,tunajua aliyokuwa akisema na kutenda , na hakuna hata siku moja aliyowahi
kuzungumzia mambo yanayohusu walemavu wa nchini kwetu.
"Kwa namna moja au nyingine sisi hatujawahi kusikia
akituzungumzia kwa namna yoyote ile, aidha akiwa bungeni au kwa waandishi wa
habari lakini kwa kuwa sasa naye ni mlemavu mwenzetu tunamkaribisha kwenye
kundi letu.Tunachomuomba afuate miongozo ya jamii ya watu wenye ulamavu ambayo
ipo na inafuatwa na waliopo kwa muda mrefu.
"Sisi walemavu wa muda mrefu ambao tumezaliwa nao
tutamuelekeza namna ya kuheshimu na kufuata miongozo iliyopo ya watu wenye
ulamavu, tunaweza kumuongoza apite wapi,atokee wapi, Kwa hiyo nadhani kwa
ukaribisho huu tunamshauri kwamba Dk.John Magufuli anatosha kusemea watu watu
wenye ulemavu, amekuwa akitutetea kwa vitendo kabla ya kuwa Rais
.Alipokuwa Mbunge,alikuwa Waziri kote huko alikuwa pamoja nasi.
Ameongeza kuwa " Na amekuwa Rais leo hii tunaona mambo
mengi ambayo yanahusu walemavu ameyaingiza kwenye mfumo wa nchi kiasi kwamba
hata atakapoondoka tutakuwa tunajua hatma yetu, sasa haya mambo mazuri hata
yeye Lissu atayafurahia.
"Hivyo ampe nafasi Dk.John Magufuli ili apeleke gurudumu
hilo mbele la mambo mazuri ya walemavu ili na sisi jamii ya Walemavu
akiwemo na yeye Lissu ambaye ameingia kwenyw jumuiya yetu basi tuweze kunufaika
wote kwa pamoja .Lissu akijitokeza kupambana na Dk.Magufuli walemavu
hatutamuunga mkono."
Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya walemavu,
amesema wanayofuraha kubwa na kutoa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa
Dk.Magufuli kutokana na kuliongoza vema Taifa la Tanzania." Tumejitokeza
hadharani kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa hotuba nzuri aliyoitoa wakati
akilifunga Bunge la 11 mjiji Dodoma.
"Katika hotuba yake amezungumzia mambo mengi mazuri
na yenye kuonesha mshikamano na umoja wa kitaifa kwa wabunge na Watanzania wote
na sisi kama jamii ya Watanzania wenye ulemavu tunamshukuru Rais wetu kwa
kuvielekeza vyama vya siasa kutujumuisha kwenye uchaguzi mkuu ujao.Rais
Magufuli tunakuahidi tutajitokeza na tutakuunga mkono,"amesema.
Ameongeza kuwa kwa CCM imeweka utaratibu mzuri ambao umeondoa
mianya ya rushwa ,hivyo ni nafasi ya watanzania kujitokeza kuwania udiwani na
ubunge.
Hata hivyo amesema watu wenye ulemavu ambao wataonesha nia zao
za kugombea kupitia vyama vyao vya siasa na pengine kuteuliwa na
kufanikiwa kushinda basi wachape kazi ili kuthibitisha uwezo wao mbele ya jamii
na iwe ishara ya kuonesha kuwa wanaweza.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Walemavu CCM John
Mlabu amesema watu wenye ulemavu wanaruhusiwa kugombea udiwani na ubunge na
katika nafasi ya Rais hiyo ni ya Dk.Magufuli tu." Uchaguzi Mkuu kwa mwaka
huu walemavu wote kura zetu kwa Rais Magufuli ,katika uongozi wake ameonesha
mapenzi makubwa kwetu na hivyo nasi tutayaonesha kwa kumpa kura."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...