Afisa Elimu wa Makumbusho ya
Taifa Bibi Anamery Bagenyi akitoa maelezo kuhusu nyayo za mwanadamu wa
kale zilizogundulika huko Laetoli katika Bonde la Olduvai.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Sokoine, Morogoro wakimsikiliza Afisa Elimu, Bibi Magreth Kigadya akitoa
maelezo kuhusu Sanaa za sasa zilizopo Makumbusho ya Taifa. Wanafunzi
hao wako katika ziara ya mafunzo jijini Dar es Salaam.

Afis Elimu wa Makumbusho ya Taifa
akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu ch Sokoine kuhusu chimbuko
la mwanadamu na zana za mawe wanafunzi hao walipotembelea Makumbusho kwa
ajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na masomo yao

Afisa wa Makumbusho ya Taifa Bw.
Ayubu Madenge akitoa maelezo kuhusu historia ya Tanzania kwa wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro walipotembelea Makumbusho ya Taifa
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza.
……………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Kilimo (SUA) wanaosomea fani ya Utalii (Tourism Management) wametembelea
Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kujifunza mambo mbalimbali
yanahusu utalii.
Wanafunzi hao ambao wako mwaka wa
pili wa masomo yao wamefika Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kujifunza
mambo mbalimbali ikiwemo mikusanyo, maonesho na vifaa mbalimbali
vinavyotumika katika maonesho.
Wanafunzi hao wapatao 203
walifika pamoja na walimu wao wawili ambapo waliweza kutembelea maeneo
mbalimbali ikiwemo kumbi za historia, chimbuko la mwanadamu, michoro ya
miamba, Sanaa za sasa na baiolojia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...