Na.Khadija seif, Michuzi tv
WAZAZI,walimu pamoja na viongozi wa kata ya Bonde la mpunga wamefanya usafi shule ya Msingi Msasani jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Michuzi tv mmoja wa wazazi waliojitokeza kwenye usafi huo Tabu perege amesema wakati mwingine wazazi wanatakiwa kujijengea mazoea ya kuwasaidia walimu pamoja na watoto kuhakikisha mazingira yanakua Safi,salama na rafiki kwaku kusomea.
"Ukizingatia watoto wetu tumekaa nao nyumbani zaidi ya miezi 3 na wiki kadhaa tangu janga hili la ugonjwa wa covid 19 (Corona) na kulazimika kupewa likizo ili kujikinga wakiwa na wazazi au walezi wao karibu na ikapelekea shule kuwa chafu kwa muda hivyo Kama wazazi tumejitokeza kusafisha maeneo yote ya hapa shuleni na agizo hilo tulipewa kupitia serikali ya mtaa wa Bonde la mpunga,"
Hata hivyo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa bonde la mpunga Mohammed Chamwana ameeleza muitikio wa wazazi kuwa umekua sio mbaya Sana na wamejitahidi kuhakikisha wanaweka mazingira Safi na salama.
"Kiufupi tulitoka agizo hili mapema na tukawataka wazazi wajitokeze kushiriki nasi usafi wa shule ili shule zinapofunguliwa watoto wao wakae mazingira Safi kusiwepo Tena na uchafu ambao utapelekea kuwadhuru na magonjwa ya mlipuko Kama kipindupindu pamoja na maralia kutokana na nyasi kuota Sana kwa kipindi cha takribani miezi mitatu waliokua nyumbani,"
Aidha,Chamwana amesema mbali na kufanya usafi wa mazingira ya shule , kupitia serikali ya mtaa wameweza kutoa ndoo 10 pamoja na vitakasa mikono kwa ajili ya watoto ili kuendelea kupiga vita ugonjwa huo wa covid 19 (Corona).
"Tuna amini bado ugonjwa upo hivyo tungependa kuendelea kuchukua tahadhari za awali kwa watoto wetu ,tumeleta vifaa hivyo ili waendelee kujikinga,"
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msasani Mw.Yera amewapongeza wazazi pamoja viongozi wa serikali ya mtaa wa bonde la mpunga kwa kuona ipo haja ya kukaribisha watoto kuanza masomo wakiwa na mazingira rafiki kwa kufundishia .
"Tuendelee kupeana ushirikiano kwenye mengine mengi tumeona mfano mzuri mmeitikia wito wa serikali yetu ya mtaa na mmekuja shuleni tumefanya usafi na ndio wakati mzuri pia wakumjua mtoto wako ana tabi gani unakuta mzazi mkaidi kufika shuleni Basi hata mtoto wake nae ana tabia za kukaidi maigizo ya walimu wake,"
Pia Yera amesema kutokana na watoto kukaa muda mrefu nyumbani ni vizuri kumuandaa tayari mtoto kwa kurudi shule kwa kuhakikisha madafatari pamoja na sare ziko safi na tayari .
"Kesho wapo watoto watakaokuja wachafu na wamechelewa ukiuliza tatizo nini huwezi pata jibu kamili hivyo ningependa wazazi waandae mapema utaratibu wa nguo zao pamoja na kuwaamsha watoto mapema,"
Mwenyekiti wa tawi la bonde la mpunga Hamad Mnyupe akiwa na torori la kuzolea takataka huku akiwa na wazazi,walimu pamoja na wajumbe wa serikali ya mtaa
Mlezi wa shule ya Msingi Msasani Salum Maguvu akitoa kiasi cha fedha shilingi laki 1 kwa ajili ya vifaa vingine vya kujikinga na ugonjwa wa covid-19 (Corona )kwa watoto pamoja na walimu wawapo shuleni jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Mohammed chamwana akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msasani B baadhi ya vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa covid 19 (Corona)
Taka zilizokusanywa na kuchomwa moto katika eneo la shule ya Msingi Msasani ikiwa Ni moja ya agizo la serikali ya mtaa wa bonde la mpunga kujitokeza kufanya usafi kabla ya kufungua shule siku ya 29.6.2020.
Baadhi ya vifaa ambavyo vimetumika kufyekea majani katika sehemu ya shule ya msingi Msasani jijini Dar es salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...