Na Editha Karlo,Buhigwe.

WANANCHI wa Wilayani Buhigwe Mkoani hapa wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwekaji umeme katika nyumba zao kwa sh.27,000 kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Akizungumza leo na wananchi walipotembelea vijiji vya Munzeze, Kishanga, Kinazi na kimara vilivyopo wilayani humo, wakati akitoa elimu ya mradi wa REA kwa wananchi, Afisa masoko kutoka Shirika la Umeme Tanzania, makao makuu Dar Es Salaam, Neema Mbuja amesema wananchi waache kujiunganishia umeme bila utaratibu kwani ni hatari kwa maisha yao.

Amesema serikali inataka kila mwananchi apate umeme na kwa kila kijiji kufikia mwaka 2025 bila kujali nyumba anayokaa kwani ni haki yake, huku akiwata kuacha tabia ya kuwatumia watu wanajulikana kama vishoka kuwaunganishia umeme na badala yake wafike katika ofisi za Tanesco zilizopo karibu nao.

“Kwa vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme waweze kuvumilia kwani hakuna kijiji kitakachorukwa bila kuwekwa umeme kwani ni haki ya kila mtanzania kupata umeme kwa bei elekezi na nafuu ya serikali ya sh.27,000”, amesema Afisa masoko wa Tanesco kutoka makao makuu Dar Es Salaam,Adelina Lyakurwa.

Afisa Uhusiano wa Tanesco, Mkoa wa Kigoma Emmanuel Matuba, amesema kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakitoa pesa zaidi ya sh.27,000 kwa watu nje ya Tanesco na kuwataka kuwekewa umeme jambo ambalo sio sahihi kwani hao wamekuwa wakiwatapeli wananchi.

Afisa usalama wa Tenesco Kigoma Khassimu Yambi, amewataka wananchi kulinda na kuitunza miundombinu ya umeme kwani serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kuijenga ili waweze kunufaika wao na vizazi vyao.
 Afisa masoko kutoka makao makuu ya Tanesco Dar Es Salaam, Neema Mbuja akitoa elimu kuhusiana na mradi wa umeme wa REA katika kijiji cha Mnazi na Kimara.
 Afisa Masoko kutoka makao makuu ya Tanesco Dar Es Salaam, Adelina Lyakurwa, akitoa elimu juu ya matumizi ya kifaa kiitwacho umeme tayari  UMETA (Ready Body), kwa wananchi wa kijiji cha Mnazi na Kimara,  kinachouzwa na shirika hilo kwa bei ya sh 36,000.
Afisa uhusiano wa Tanesco mkoa wa Kigoma, Emmanuel Matuba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Munzeze,Kishanga vilivyopo wilayani Buhigwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...