Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imemtia hatiani na kumhukumu kulipa faini ya Shilingi Milioni 5 au kifungo Cha Mwaka mmoja jela Mwandishi wa habari Prosper Mfugale baada ya mwandishi huyo kukiri kutoa maudhui Katika Mtandao wa YouTube bila ya kuwa na leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), hata hivyo Mfugale amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Mfugale alikamatwa mnamo Februari 29 Mwaka huu na kushikiliwa kwa siku nne kituo cha polisi Njombe na tarehe 4 Machi alifunguliwa mashitaka ya kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kinyume cha Sheria ya Maudhui Mtandaoni ya mwaka 2018.
Wakili Chance Luoga kutoka mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania alikuwa anasimamia Kesi yake tangu alipokamatwa.
(Watetezi TV)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...