WANAOMPINGA RAIS MAGUFULI WANA URAIA WA NCHI MBILI-MASAUDA

Masauda
akizungumza jana mjini Babati alisema yeye alikuwa mjumbe wa mkutano
mkuu wa CCM Taifa mwaka 2007 hadi 2015 hivyo anashangazwa na vigogo kama
Bernard Membe wanampinga Rais Magufuli.
Alisema
wanaompinga wanapaswa kutambua kuwa Rais Magufuli anapaswa kupita bila
kupingwa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
ili aone namna anavyoungwa mkono na watanzania na siyo kupingwa.
Alisema
Membe hana uwezo wa kipambana na Rais Magufuli, kwani hata kwenye
mkutano mkuu wa Taifa Dodoma mwaka 2012 alishindwa kwa kura na Januari
Makamba na Mwigulu Nchemba kati ya watu 12 waliopitishwa NEC Membe
alikuwa wa saba.
"Wewe
kama ulishindwa na kina January na Mwigulu utamuweza Rais Magufuli hata
akisimama na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira kwa kweli
atagaragazwa kwani Rais Magufuli ni wa kwanza kukubalika na wakulima na
wafugaji," alisema.
Alisema
hata Membe akiachiwa aingie uwanjani hivi sasa hana mvuto Rais Magufuli
ni mzalendo atamuacha mbali sana hivyo asijisumbue aachane na wazo hilo
la kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Aliwataka
vijana wachangamkie fursa ya kugombea ubunge na udiwani kwani Rais
Magufuli ameirudisha CCM katika misingi bora na hata usipokuwa na fedha
hivi sasa unaweza kugombea uongozi.
"Vijana
changamkieni fursa hata ukiangalia mwaka 2015 fomu za kugombea ubunge
ndani ya CCM ilikuwa shilingi milioni 2.1 na hivi sasa ni sh100,000 ni
ishara tosha kuonyesha kililenga matajiri sasa hivi chini ya Rais
Magufuli ni chama cha wanyonge," alisema Masauda.
Alisema
vijana wasijali lolote kwani CCM chini ya uenyekiti wa Rais Magufuli na
Katibu Mkuu Dk Bashiru Ally imekuwa mpya na kimbilio la watu wanyonge
tofauti na awali.
Alisema
vijana wanachangamkia fursa kwani hata hivi sasa mjini Babati watia nia
ya kugombea ubunge ndani ya CCM wapo zaidi ya 20 wakiwemo walimu 12 na
madaktari sita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...