Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango ameomba msamaha ili kutoa ushuhuda ushuhuda wake kuhusu Rais Dk.John Magufuli ambapo amesema Baba huyu(Dk.Magufuli) ni kiongozi mwenye maono na uwezo mkubwa.
Aidha, ana kipaji cha hali ya juu cha kufanya yasiyowezekana na ni kiongozi ambaye anafahamu vema kuwa ili nchi ifanikiwe kuleta mabadiliko chanya ni lazima kuvunja kabisa utaratibu wa kufanya kila kitu kwa mazoea (break the status quo in order to break through).
Dk.Mpango ameyasema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati anahitimisha hotuba ya bajeti ya Fedha ya mwaka 2020/2021 ambapo amemuelezea Rais Magufuli kuwa ni jemadari anayetambua vema kwamba bila jasho hakuna tuzo na huu ndiyo msingi wa kauli mbiu ya HAPA KAZI TU!
"Ni kiongozi jasiri ambaye anajiamini na ana ndoto kubwa kwa maendeleo ya nchi (has no room for small dreams), tena hana woga wa kushindwa. Kwa sababu hizo amekuwa akituasa watanzania tubadilike na kujiamini. Kwa maneno yake mwenyewe amekuwa akituambia "watanzania tunaweza, Tanzania siyo masikini". 125.
"Tangu mwanzo wa utawala wake Rais Magufuli amepambana na rushwa na ufisadi bila kigugumizi. Amevunjavunja mazoea ya udanganyifu uliokuwa umekithiri kila kona kama vile watumishi hewa, mishahara na posho kwa watumishi vizuka, mikopo kwa 140 wanafunzi ambao hawapo, madai ya kugushi ya pembejeo na marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani. Rais huyu ni mfuatiliaji makini, tena kwa takwimu, wa kila kinachoendelea katika kila eneo la utawala.
"Rais Magufuli alijipa kazi ya kutumbua majipu na ameifanya kazi hiyo bila kupepesa macho ndani ya Serikali na hata ndani ya CCM. Ni dhahiri kwangu kuwa Rais Magufuli ni muumini wa mafundisho ya uongozi ya Peter Ferdinand Drucker (ingawa sina hakika kama Rais wetu alisoma maandishi ya mtaalam huyo mashuhuri) kwamba, naomba kunukuu kwa Kiingereza,"amesema.
Ameongeza kuwa Rais Magufuli ni kiongozi wetu mkuu ambaye amesimamia kwa karibu nidhamu ya matumizi katika wizara, idara na taasisi za Serikali Kuu na 141 Mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kudhibiti safari za watumishi wa umma nje ya nchi, hata yeye mwenyewe hajasafiri nje ya Bara la Afrika tangu alipochukua hatamu za uongozi wa nchi hadi sasa; amefuta baadhi ya sherehe za kitaifa na kuelekeza fedha zilizokuwa zimepangwa zitumike kwenye maeneo mengine yenye uhitaji mkubwa; na alipiga marufuku "MKUKUBI".
Kwa wasiofahamu MKUKUBI ni kifupi cha kilichokuwa kinaitwa kininja kama 'Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Binafsi' kupitia posho za kwenye makongamano, semina na warsha zilizokuwa zinafanyika kwenye kumbi za kukodi na hoteli.
Aidha, alipunguza misafara mirefu ya kusindikiza viongozi kwenda kwenye matibabu au kupima afya zao nje ya nchi huku wakiacha hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali za rufaa nchini zikiwa zinadidimia. Mtakumbuka pia alichukua hatua isiyotarajiwa ambayo iliduwaza watu wengi na hata kupelekea wengine kumlaumu pale alipoamua kumpeleka mke wake (First Lady) hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu ambapo alilazwa kwa siku kadhaa badala ya kumpeleka nje! 127.
" Rais Magufuli ni Jemadari mwenye msimamo usiotetereka hata 142 kwenye kilele cha hatari (crisis) kama wakati wa malalamiko kuwa "vyuma vimebana", pia katika kipindi cha uhaba wa mafuta ya kula na hivi karibuni wakati watawala wengine wakilazimisha wananchi wao kubakia majumbani (Lock down) ili kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID - 19), kwa mshangao wa wengi Rais Magufuli aliagiza watanzania waendelee kuchapa kazi, na wazingatie maelekezo ya wataalam wa afya kujikinga na CORONA huku wakiendelea kumwomba Mungu!
" Aidha, katika nafasi yake ya Amiri Jeshi Mkuu, ameendelea kiliamini Jeshi, kulijengea uwezo na kulishirikisha katika miradi mbalimbali ya kimkakati ya ujenzi wa uchumi wa nchi yetu. 128. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha utawala wake Rais Magufuli ameendelea kumtanguliza Mungu katika kazi zake na kuwaelekeza viongozi anaowateua na wananchi kwa ujumla nao wafanye hivyo hivyo.
"Ameonesha unyenyekevu na ukarimu sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuenzi mchango wa awamu za uongozi zilizotangulia, kuchangia ujenzi wa nyumba za ibada (misikiti na makanisa), kukusanya sadaka kanisani yeye mwenyewe, kushiriki misiba ikiwa pamoja na ile inayogusa 143 viongozi wa vyama vya upinzani, kutembeza sinia lenye vitafunio vya chai pale ikulu Dar es Salaam na Chamwino kwa ajili ya wageni wake, na kunywa kahawa au kununua bidhaa na matunda kutoka kwa wajasiriamali wadogo. Rais Magufuli ana huruma na anaumizwa na kilio na machozi ya wanyonge au waliodhulumiwa na hasiti kuwafuta machozi hapo hapo.
"Ni kwa mantiki hiyo kiongozi wetu huyu amewatembelea wafungwa magerezani kujionea hali halisi na kuongea nao na kufanya uamuzi wa kusamehe idadi kubwa sana ya wafungwa na mahabusu. Kama hiyo haitoshi, baba huyu ameendeleza moyo wake wa msamaha hata kwa waliombeza na kumtusi! 129.Kiongozi wetu mkuu ni mzalendo namba moja ambaye amevaa koti la Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na kufufua ndoto zake za maendeleo ya Taifa letu,"amesema Dk.Mpango wakati anamueleza Rais Magufuli.
Pia alianza kwa kupiga vita rushwa na ukwepaji kodi vilivyokuwa vimekithiri bandarini na TRA na kufanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato ya kodi kutoka wastani wa shilingi bilioni 825 kwa mwezi kabla ya utawala wake hadi wastani wa shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi katika mwaka 2019/20. Aidha alielekeza mikataba ya madini na huduma muhimu kama mawasiliano ipitiwe upya 144 na kutunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 ili kulinda rasilimali za Taifa na kuhakikisha watanzania wananufaika.
Rais Magufli pia amejenga uzio wenye urefu wa kilometa 24.5 kuzunguka mgodi wa madini ya tanzanite Mirerani na kuanzisha masoko ya madini; Aidha, aliamua kutekeleza maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha TANU kilichofanyika tarehe 30 Agosti hadi tarehe 1 Septemba mwaka 1973 kuhamisha makao makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam kuja hapa Dodoma. 130. Rais wetu John Magufuli amethubutu kutekeleza miradi mikubwa ya kielelezo iliyobuniwa na Baba wa Taifa ikiwa ni pamoja na bwawa la Nyerere la kuzalisha umeme wa MW 2,115 katika mto Rufiji.
Pia kujenga uchumi wa viwanda; kujenga reli ya kati ya kisasa (Standard Gauge Railway); kufufua Shirika la Ndege la Tanzania kwa kununua ndege mpya 11 na kujenga viwanja vya ndege; kuendeleza ujenzi wa barabara kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa; kununua meli mpya za abiria na mizigo na kukarabati zile za zamani na vivuko pamoja na kupanua au kuboresha 145 bandari katika ukanda wa bahari na maziwa makuu; kutoa elimu hadi kidato cha nne bure.
Dk.Mpango amesema Rais Magufuli ameongeza mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu; mradi kabambe wa kupeleka umeme vijijini (REA) ambapo hadi sasa vijiji 9,112 kati ya vijiji 12,268 vya Tanzania Bara (asilimia 74.3) vimeunganishiwa umeme; ameendelea kupiga vita adui maradhi kwa kuimarisha huduma za afya nchini kama ilivyoelezwa kwa kirefu katika taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa niliyosoma leo asubuhi. 131. Mheshimiwa Spika, Rais wetu huyu ana akili ya kisayansi ya kudadisi na kuhoji kila jambo ikiwa ni pamoja na usahihi wa vipimo vya mafuta ghafi ya kula na hata ugonjwa wa CORONA.
" Rais Magufuli amekuwa mfano bora wa kutumia na kuenzi lugha ya kiswahili hata kufikia kuwa moja ya lugha zilizokubalika kutumika katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC. 132. Mheshimiwa Spika, Rais Magufuli ni kiongozi anayetuhimiza watanzania kuwa wamoja na kusisitiza kuwa maendeleo hayana chama. Rais Magufuli ana nidhamu kubwa ya kufanya kazi,"amesema.
Ametumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzaia kumpa zawadi ya kura ya Ndio Rais huyu ambaye amekuwa mfano wa kuigwa na wa kipekee katika bara la Afrika kama shukrani yetu kwake kwa kazi yake iliyotukuka ili aendelee kuipaisha nchi yetu ya Tanzania kwa kipindi cha pili cha miaka mitano.
"Watanzania msisahau pia kumpatia Rais wetu wabunge na madiwani wanaomudu maadili na mwendo wa HAPA KAZI TU, na kama itawapendeza wananchi wenzangu wa Buhigwe na Chama chetu, basi iwe pamoja na mimi mtumishi wenu! Nawaambia kweli watanzania wenzangu, Rais huyu ni tunu ya thamani kubwa kwa Tanzania na utawala wake ni fursa kubwa ambayo kama hatutaitumia vizuri, basi mjue itachukua 148 miaka mingi ijayo kuifikia Tanzania mpya tunayoitamani.
"Na kwa mheshimiwa Rais, najua unafuatilia hotuba hii, sina maneno mazuri ya kukushukuru kwa kuniinua, kunipa heshima kubwa ya kulitumikia Taifa katika Serikali yako na kwa kuniongoza vizuri katika utumishi huu. Mwenyezi Mungu akubariki, akulinde, akufadhili na kukupa amani wewe na familia yako".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...