Na Said Mwishehe ,Michuzi TV

KATIKA kuendelea kukabiliana na virusi vya Corona nchini, SerikaIi kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imepokea msaada wa matanki 100 kutoka kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya umeme ya AFRICAB maalumu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi na wanavyuo jijini Dar es Salaam kunawa mikono ili kukabiliana na janga la homa mapato inayosababishwa na virusi vya Corona.

Akipokea na kisha kukabidhi matanki hayo yenye thamani ya Sh. Milioni 50, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako mbali na kushukuru kwa msaada huo, amefafanua kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo vyuo na baadhi ya shule nchini zimefunguliwa na itawawezesha wanafunzi kujikinga dhidi ya ugonjwa huo wa Covid-19.

Ameongeza kuwa msaada wa matanki hayo yenye ujao wa lita 1000 kila moja yametolewa kwa shule 10 za Sekondari za Serikali na 57 kwa shule za sekondari za binafsi na vyuo 13 ni muhimu kwa Serikali hasa wakati huu ambapo vita dhidi ya ugonjwa huo unaendelea.

Profesa Ndalichako amesema kuwa "Naiwapongeze AFRICAB msaada huu muhimu kwa ajili ya kinda afya za wanafunzi wetu, niwaombe wadau wengine muige mfano huu kwa ajili ya manufaa ya watu wote wa taifa hili,"amesema Prof.Ndalichako na kuongeza licha ya hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika napambana dhidi ya Corona, wananchi nao wanapaswa kuchukua tahadhari hizo huku wakiendelea kuchapa kazi.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa AFRICAB David Tarimo, ametumia nafasi hiyo kueleza msaada umetolewa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na Corona na kusisitiza kuwa wao kama wadau wa maendeleo na wawekezaji wazalendo huo ni wajibu wao wa kimsingi.

"Mapambano dhidi ya Corona ni wajibu wa kila mmoja wetu na sisi AFRICAB tunatambua nini kinafanywa na Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo unaoisumbua dunia kwa sasa.Aidha mbali na msaada huo, AFRICAB itaendelea kushirikiana na Serikali katika masala mbalimbali ya kimaendeleo huku ikitarajia kujenga cha uzalishaji wa dawa za binadamu hivi karibuni " amesema.

Awali Mkurugenzi Mwenza wa kiwanda hicho Mohammed Ezz amesema kwamba anatoa shukrani za dhati kwa Rais John Magufuli kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji yanayokiwezesha kiwanda hicho kutekeleza majukumu yake ipasavyo." Tunamshukuru Rais Magufuli kwa namna ambavyo ameweka mzingira mazuri ya uwekezaji na hii imekuwa fursa kwetu kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia ubora ww viwango vinavyotakiwa."

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe uzindua ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kwa lengo la  kupambana na maambukizi ya Corona. Aliyeambata naye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Africab.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akizungumza baada ya kukata utepe kuashiria  uzinduzi wa ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kupambana na maambukizi ya Corona. Kulia kwani ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na Wakurugenzi watendaji wa Kampuni ya Africab.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako akikagua moja ya tanki la maji kati ya mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yaliyotolewa na kampuni ya Africab kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam kupambana na maambukizi ya Corona.

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa kampuni ya Africab baada ya kuzindua ugawaji wa mataki 100 ya kunawia mikono yenye thamani ya shilingi milioni 50 yalitolewa na kampuni hiyo  kwa Shule na Vyuo vya jijini Dar es Salaam ili kupambana na maambukizi ya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...