Na Woinde Shizza ,Michuzi Tv Arusha
Mchakamchaka wa kuomba ridhaa Ndani
ya Chama Cha mapinduzi kwa nafasi ya ubunge na udiwani umefunguliwa
huku zaidi ya wagombea ubunge 30 wakijitokeza kwa nyakati tofauti
kuchukuwa fomu katika Jimbo la Arusha mjini
Akizungumza
wakati wa Zoezi la kuchukuwa fomu katika makao makuu ya Chama hicho
wilayani hapa Katibu wa CCM Wilaya Arusha Denis Mwita Zakaria amesema
kuwa uchukuaji wa fomu utaenda sambamba na maagizo ya Chama kwa Kila
mmoja kufuata taratibu.
Alisema
kuwa msingi na maadili ya Chama hicho kwa wagombea hadi kwenye siku ya
mchujo yahitajika kuzingatiwa kwa waombaji wote Ndani ya CCM hivyo kila
moja anao wajibu wa kufuata maagizo hayo ikiwemo kutotoa rushwa Wala
kuanza kampeni mapema.
"Niwaombe
Sana wagombea kuendelea kuchukuwa fomu na kusubiria maelekezo ya Chama
kwa kufuata utaratibu kanuni na maadili kwa wagombea wote ikiwemo
kukwepa vitendo vya rushwa wakati wote wa uchaguzi wa Ndani ya Chama
hicho pamoja na kutochezeana rafu"
Awali
baadhi ya wagombea akiwemo meya mstaafu wa jiji la Arusha Kalist Lazaro
aliyechukuwa fomu mchana alisema kuwa ametumia haki yake ya kikatiba
kuchagua na kuchaguliwa ndio vilivyomsukuma kuomba nafasi hiyo.
Nae
Mrisho Gambo alisema kuwa Kuna mengi yanamsukuma kuomba nafasi hiyo
hivyo watu wasubiri muda utaongea hapo usoni kwani ana imani na vikao vya
Chama hicho kuweza kuleta mgombea anayekubalika atakayepeperusha
bendera ya Chama hicho katika Jimbo la Arusha.
Kwa
upande wake Philemon Mollel alisema kuwa anayoimani kubwa ndio maana
akaamua kuchukuwa fomu kuomba Chama hicho kumpitisha kugombea nafasi
hiyo hivyo wasubiri vikao kwa Sasa Sina zaidi ya haya.
Katika
ofisi za Wilaya ya Arusha za Chama hicho wagombea kadhaa wamekuwa
wakipishana kuchukuwa fomu za kuomba Chama hicho ridhaa ya kupata nafasi
ya kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CCM.
Hatua
hiyo inaleta kuwepo kwa mvutano mkubwa wakati wa kura za maoni na
kukifanya Chama hicho kuweza kumpata mgombea atakayekwenda kupambana na
mgombea wa vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu mwezi November.
Mgombea Ubunge wa
Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Arusha mjini ambaye ni Mwanamama wa kwanza
kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo Hilo Anna Mwambapa akipokea
fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikabidhiwa fomu ya kugombea
nafasi ya ubunge Jimbo la Arusha mjini leo kutoka kwa katibu wa Chama Cha
Mapinduzi Denis Mwita ,mgombea huyo alisindikizwa na familia yake
kwenda kuchukuwa fomu katika ofisi za CCM Wilaya zilizopo Wilaya ya
Arusha (picha na Woinde Shizza,ARUSHA)
Mfanyabiashara
Maarufu jijini Arusha Philemon Mollel (Monabani) akikabidhiwa fomu ya
kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha mjini na katibu wa CCM Wilaya ya
Arusha mjini Denis Mwita
Katibu
wa CCM Wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi Victor Mollel fomu ya
kugombea ubunge Jimbo la Arusha mjini .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...