Na Shukrani Kawogo, Njombe.
 
Baadhi ya watendaji wa serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa, wapigana vikumbo katika ofisi za chama hicho wilayani Ludewa mkoani Njombe kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania ubunge katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Wamechukua hatua hiyo baada ya Chama hicho kutangaza kuanza kutoa fomu hizo leo kwa wanachama wake wanaotaka kuteuliwa na chama hicho kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini kwenye uchaguzi huo utakaovishirikisha vyama vingi vya siasa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa CCM wilaya Bakari Mfaume amesema kuwa katika siku ya kwanza ya uchukuaji fomu wamejitokeza wagombea 12 huku mmoja kati yao Dk. Primius Nkwera amejaza na kurudisha.

Hata hivyo kwa upande wa katibu wa wanawake (UWT) wilayani humo Flora Kapalia amesema katika siku ya kwanza amepokea wagombea 19.

Zoezi hilo linafuta baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata wagombea wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Dk. Hussen Mwinyi kwa Zanzibar katika vikao vya chama hicho vilivyomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita. 
 Mhadhiri wa chuo cha Tumaini Arusha akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Ludewa na katibu wa CCM Wilayani humo Bakari Mfaume
 Aliyekuwa katibu mtendaji wa baraza la elimu na vyuo vya ufundi (NACTE) Dk. Primius Nkwera akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Wilayani humo Bakari Mfaume
 Kamishna msaidizi wa ardhi mkoa wa Dodoma, Joseph Kamonga akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Ludewa na katibu wa CCM Wilayani Ludewa Bakari Mfaume
Mwanasheria mwandamizi mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Philipo Filikunjombe akichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Ludewa na katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa Bakari Mfaume.
 Aliyewahi kuwa Kamishna wa jeshi la Polisi pia katibu Tawala mkoa wa Mwanza Clodwig Mtweve akichukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea ubunge jimbo la Ludewa
 Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk. Luka Nkonongwa akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya ubunge jimbo la Ludewa na katibu wa CCM Wilayani Ludewa
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...