Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine Musisi - Mwakilishi Mkazi mara baada ya kukamilika kwa kikao cha mashirikiano baina yao. Wengine katika picha ni wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na UNDP.
Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akisalimiana na Bi. Christine Musisi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya mkutano baina yao uliofanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba - Dodoma. Pamoja na mambo mengine mkutano huo umejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira.
Balozi Joseph Sokoine Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia) akiwa katika kikao pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ukiongozwa na Bi. Christine Musisi ambae ni Mwakilishi Mkazi. Kikao hicho kimelenga kuimarisha ushirikiano katika hifadhi ya Mazingira hususan katika maeneo ya Mabadiliko ya Tabianchi, Uchumi wa Bahari, Nishati endelevu, Hifadhi ya Bioanuai na Ikolojia. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Makamu wa Rais Mtumba - Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...