Meneja Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Kanda ya Ziwa, Usama Choka (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita Philip Shoni
wakati walipofika Ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya
kuanza zoezi la utoaji elimu kuhusu mwongozo wa uombaji mikopo ya elimu
ya juu kwa Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na Stashahada Wilayani
humo. Kulia ni Afisa Mikopo wa HESLB Jonathan Nkwabi. Mafunzo hayo
yalifanyika leo Jumatano (Julai 29, 2020) katika shule ya Sekondari
Chato. Mkoani Geita
Maafisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu ya Juu (HESLB) wa pili
kutoka kushoto Usama Choka, Winfrida Wumbe na Jonathan Nkwabi wakiwa nje
ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato muda mfupi kabla ya kuanza
kuanza zoezi la utoaji elimu kuhusu mwongozo wa uombaji mikopo ya elimu
ya juu kwa Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na Stashahada Wilayani
humo. Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano (Julai 28, 2020) katika
shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chato, Benard Majura (katikati)
akifurahia jambo kwa pamoja na Maafisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB) muda mfupi kabla ya kuanza zoezi la utoaji elimu
kuhusu mwongozo wa uombaji mikopo ya elimu ya juu kwa Wanafunzi
waliohitimu kidato cha sita na Diploma Wilayani humo. Mafunzo hayo
yalifanyika leo Jumatano (Julai 29, 2020) katika shule ya Sekondari
Chato Mkoani Geita.
Meneja Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Kanda ya Ziwa, Usama Choka akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita
katika Shule ya Sekondari Chato na Shule ya Wasichana ya Jikomboe pamoja
na wahitimu wa masomo ya kidato cha Sita katika shule mbalimbali
Wilayani Chato wakati wa zoezi la utoaji elimu kuhusu mwongozo wa
uombaji mikopo ya elimu ya juu kwa Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita
na Stashahada Wilayani humo. Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano
(Julai 29, 2020) katika shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Meneja Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Kanda ya Ziwa, Usama Choka (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita Philip Shoni
wakati walipofika Ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya
kuanza zoezi la utoaji elimu kuhusu mwongozo wa uombaji mikopo ya elimu
ya juu kwa Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na Stashahada Wilayani
humo. Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano (Julai 29, 2020) katika
shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Afisa Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Jonathan Nkwabi akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na
wahitimu wa masomo ya kidato cha Sita na wanafunzi wanaoendelea na
masomo ya kidato hicho wakati wa zoezi la utoaji elimu kuhusu matumizi
ya mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa
masomo 2020/2021. Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano (Julai 29, 2020)
katika shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Baadhi ya wahitimu wa masomo ya kidato cha sita katika shule mbalimbali
Wilayani Chato Mkoani Geita wakifuatilia kwa makini mafunzo
yaliyotolewa na Maafisa wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kuhusu
matumizi ya mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa
mwaka wa masomo 2020/2021. Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano (Julai
29, 2020) katika shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu Arusha, Mahila Matulo
akichangia hoja wakati wa wakati wa zoezi la utoaji elimu kuhusu
matumizi ya mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa
mwaka wa masomo 2020/2021 lililoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu (HESLB). Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano (Julai
29, 2020) katika shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Baadhi ya Walimu Wakuu wa Shule mbalimbali za Sekondari Mkoani Geita
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu (HESLB) muda mfupi baada ya kumalizika kwa mafunzo ya
kuhusu matumizi ya mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu kwa mwaka wa masomo 2020/2021 lililoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB). Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano
(Julai 29, 2020) katika shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita.
Afisa
Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu ya Juu (HESLB) Jonathan
Nkwabi akitoa ufafanuzi wa wa hoja mbalimbali zilizotolewa na wahitimu
wa masomo ya kidato cha Sita na wanafunzi wanaoendelea na masomo ya
kidato hicho wakati wa zoezi la utoaji elimu kuhusu matumizi ya mwongozo
wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo
2020/2021. Mafunzo hayo yalifanyika leo Jumatano (Julai 29, 2020) katika
shule ya Sekondari Runzewe, Bukombe, Mkoani Geita.
(PICHA NA BODI YA MIKOPO -HESLB)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...