Watanzania
wametakiwa kulisemea mambo mazuri Taifa lao ili kuwa na kidiplomasia
nzuri na Mataifa mengine hususani wakati huu ambapo Taifa linaomboleza
kifo Hayati Benjamini William Mkapa na kuachana na habari za upotoshaji
zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii hasa baada ya ujumbe wa Kenya
uliokuwa ushiriki katika maziko ya kitaifa Jijini Dar Es Salaam
kushindwa kufika kama ilivyokuwa imepangwa
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Damas
Ndumbaro ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kufuatia kuenea taarifa za
uzuishi katika mitandao ya kijamii hususani baada ya ujumbe uliokuwa
uiwakilishe Kenya katika maziko ya kitaifa yaliyofanyika Uwanja wa
Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kushindwa kufika na ndege iliyokuwa
imewabeba wajumbe hao kurejea Kenya.
Dr.Ndumbaro
ameongeza kuwa kuandika au kuchapisha taarifa za uzushi na zisizo na
uthibitisho ni kinyume cha sheria za mitandao yam waka 2015 na adhabu
yake ni pamoja na kifungo gerezani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...