MKUU wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo amemsifu mbunge wa jimbo la Chalinze Ndg Ridhiwani Kikwete kwa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi(CCm) kwa asilimia 98% kwenye miradi mbalimbali kwa ajili ya wananchi.

Akizungumza na Mbunge ofisini Kwake wakati alipokuwa akikabidhiwa vitabu vya taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkuu wa Mkoa huo wa Pwani Mwandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa Chalinze imekuwa ya mfano katika kufanikisha usimamizi wa  miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na serikali Kuu, Tamisemi kupitia halmashauri hiyo na mingineyo inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi na wafadhili walioshawishiwa na mbunge wa jimbo hilo. 

Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana kwa ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, Ujenzi wa Miundo mbinu ya umeme takribani kila kijiji,miundombinu ya barabara kuhakikisha kuwa zinapitika muda wote, kupatikana kwa maji na mabadiliko ya uendeshaki wa shughuli za upatikanaji wa Maji kiurahisi na uimarishaji wa Elimu, upatikanaji wa Mamlaka kamili ya Wilaya ya Chalinze ni kwa sehemu kubwa Mchango wa Mheshimiwa Mbunge ambao unatokana na mahusiano makubwa ambayo yamejengwa na Mheshimiwa Mbunge akishirikiana na Serikali katika kuhakikisha Wananchi wake wanapata faida ya kuchagua Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Aliongeza kuwa Kikwete amekuwa kiunganishi kikibwa baina ya serikali na wananchi kwani amekuwa akiwasemea sana Wananchi wake  bungeni na kubisha hodi ofisi mbalimbali za Serikali hasa kwangu na za mawaziri kwa lengo la kujua jimbo lake linafaidikaje na Fursa zilizopo.

"Katika mkoa wangu wa Pwani jimbo la Chalinze ndio limekuwa la kwanza katika utekelezaji wa ilani ya CCM kutokana na kile ambacho tulikuwa tukikihitaji kifanyike kimefanyika na wananchi wanaendelea kutumia miradi hiyo"Alisema Eng Ndikilo.

Aidha alisema kuwa utekelezaji huo uliofanywa na Mh.Kikwete umepelekea kutatuliwa kwa changamoto mbalimbali za wananchi wa maeneo hayo hivyo kuleta mafuu sio tu ya kiutendaji bali pia ya maisha ya watu na biashara hasa za mazao katika halmashauri ya Chalinze. Katika nasaha nyengine za Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi hao wa Chalinze kutumia fursa hiyo ya uwepo wa miradi hiyo kujinufaisha ili waweze kupata maendeleo.

Kwa upande wa Mlezi wa Mkoa huo , Mama Gaudensia Kabata Ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakinamama wa Chama Cha Mapinduzi alimpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi Nzuri ambayo inayoa nafasi kwa wagombea wa chama kujinadi bila wasi wowote. Lakini kwa upekee kabisa alimshukuru sana kwa msaada mkubwa aliputoa kuhakikisha jamii ya kifugaji inarudi kwenye amani kwa kurudisha Kijiji, kuwahangaikia eneo la malisho na kuwezesha kuanza kwa majadiliano ya kupungua gharama ya kukodisha vitalu.

Mlezi huyo aliongeza kuwa Zinapofanyika kazi nzuri kama hizo ni muhimu jamii kutambua kuwa watu wanahangaika kwa ajili yao na mheshimiwa Mbunge ni mfano mzuri wa kuigwa katika kutekeleza haya."Ninampongeza sana Mbunge Kikwete kwa kazi Nzuri aliyoifanya ambayo inamuhakikisha hata Mgombea wetu wa Nafasi ya Uraisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupata Kura nyingi sana. Hongera sana na Ninakupongeza na kukushukuru sana Mheshimiwa Mbunge", alimaliza.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya mstaafu wa wilaya ya Kibaya Assumter Mshama amempongeza mbunge huyo kwa uchapakazi wake uliotukuka kwa wananchi wake na kumtaka kuendelea na moyo huyo kwani wananchi ndio wanajua walipokuwa siku za nyuma na walipo sasa kwani kila yaliyofanyika katika jimbo hilo analoliongoza yanaonekana wazi.

Naye mbunge wa jimbo hilo Mh Ridhiwani Kikwete amewashukuru viongozi hao kwa kumpa moyo kwa kile alichokiita kazi kubwa iliyokwisha fanyika katika jimbo hilo. Aliendelea kusisitiz na kushukuru msaada mkubwa anaopewa na Mheshimiwa Raisi na Serikali yake.

Mheshimiwa Mbunge alikumbusba kuwa kama isingalikuwa mafiga matati ya ushirikiano isingeliwezekana haya. Aliongeza kuwa utekelezaji uliofanyika chalinze ni shirikishi baina ya nguzo tatu ambazo ni wananchi, wawakilishi na serikali.

Aidha Kikwete amemsifu Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa nguzo yake katika ufanikishaji wa maendeleo kwenye jimbo la chalinze hasa katika kukabiliana na changamoto za wananchi katika wilaya yao na pia kusisistiza wananchi wajiandae kwa ajili ya yanayokuja ambayo ni makubwa sana . 

"Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt Magufuli imekuwa bega kwa bega na Chalinze ndio maana imetupatia fedha nyingi kwenye miradi mbalimbali inayolenga kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero zilizokuwa zikiwasumbua awali"Alisema Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...