NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU
wa wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Zainab Kawawa, ameagiza Kampuni ya
Kijiko pamoja na wananchi wa Kijiji cha Kiharaka kutoliendeleza eneo
hilo lenye hekari 100, mpaka watakapopewa maelekezo ya Serikalini.
Aidha
ameshangazwa na Serikali ya Kijiji hicho kutoa ardhi hekari 100 kwa
Kampuni hiyo, kwa lengo la kujenga nyumba za bei nafuu wakati mpaka sasa
hakuna ujenzi wowote, na kwamba Kijiji uwezo wake wa kutoa ardhi mwisho
hekari 50.
Kawawa alitoa
kauli hiyo ,kijijini hapo alipokwenda kusikiliza kilio cha wakazi
waliolalamikia kuwepo kwa zoezi la upimaji ardhi na kuwekwa mawe wakidai
kwamba eneo lao tayari limepimwa, huku wananchi wakiwa na hati ya
kumiliki, ambapo wanashangazwa na zoezi hilo.
Alieleza
,amepata taarifa ya mgogoro ulioanzia mwaka 2000 na 2010, kampuni ina
nyaraka zinazoonyesha hati, wakati pia kwa wananchi wanaonesha hati za
maeneo yao.
Baadhi
ya wakazi Sharifa Salehe, AllyMan Mohamed na Marrey Abdallah
wàmeshukuru kwa namna Kawawa anavyofuatilia kwa karibu sakata hilo .
"Tunaishukuru
Serikali ya wilaya chini ya Mkuu wetu Zainab Kawawa kwa jitihada zake
kuhusiana na mgongano huu, pia tunamuomba Rais Dkt. John Magufuli
aliingilie suala letu kwani limeshakwenda Mahakamani tukashinda lakini
bado tunaendelea kusumbuliwa," alisema Sharifa.
Mmoja
wa vijana wa wamiliki wa ardhi hiyo ya hekari 100 ,Marrey ameviomba
vyombo vinavyofuatilia suala hilo visimamie kwa umakini ili waweze
kupata haki yao ya kimsingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...