Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya yake ambapo leo amekagua ujenzi wa Daraja la Mseta, Kituo cha Afya Chamkoroma na Kituo cha Afya Mlali ambapo miradi yote jumla inagharimu Sh Milioni 850.

Katika ziara hiyo ya ukaguzi DC Ndejembi ameambatana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ili kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ndani ya miaka minne na kusema kuwa maendeleo yote yamefanyika kwa sababu ya kuwa na  Kiongozi mwenye maono, spidi ya kazi na uzalendo, na kuwasihi watanzania kumuunga tena mkono kwa miaka mitano mingine.

Amesema maendeleo yanayofanyika Kongwa na Nchi nzima kwa ujumla kama ingekua ni Kiongozi mwingine angeweza kutumia miaka 12 lakini Rais Magufuli ametumia miaka minne tu kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati na kutoa rai kwa watanzania kutokubali kumpoteza kirahisi Rais Magufuli kwa kudanganyika na Siasa za wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania badala yake wamuunge mkono tena kwenye uchaguzi mkuu ujao ili azidi kuleta maendeleo.

" Fikiria juzi tumetembelea miradi mingine Kata ya Mkoka huko ambapo zaidi ya Bilioni Moja imetumika kwa ajili ya Vituo vya Afya na miradi ya Maji, leo tumetembelea hapa zaidi ya Milioni 800 zimetumika kwenye Afya na Daraja, Kongwa tuna kila sababu ya kuishukuru serikali yetu kwa kazi kubwa wanayotufanyia.

Ni ngumu sana kuona Nchi moja inatekeleza kwa ufasa miradi mikubwa tena mingine ya kimkakati kwa wakati mmoja na zaidi wakitumia fedha zao za ndani, sisi Tanzania ni mfano wa Nchi hiyo. Niwasihi tena watanzania kumuunga mkono Rais wetu kwa kumpigia kura nyingi za ndio na kwa wananchi wenzangu wa Kongwa kura ya Mbunge mhakikishe mnaipeleka kwa Spika wetu Job Ndugai ili azidi kushirikiana na serikali yetu kutuletea maendeleo, " Amesema DC Ndejembi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akitoa maelekezo ya mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Chamkoroma mbele ya Kamati ya Siasa ya Wilaya.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...