Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imesema imetenga zaidi ya Sh Milioni 870 ili kuwaendeleza wabunifu na bunifu zao kwa maendeleo ya binafsi lakini pia kwa Taifa lengo likiwa kuthamini vipaji na ubunifu walionao watanzania.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa mwaka huu.
Washindi hao wa ngazi mbalimbali wametunukiwa vyeti vya ushindi na zawadi ambapo mshindi wa kila kundi amezawadiwa Sh Milioni Tano, wa pili Sh Milioni Tatu na wa tatu Sh Milioni mbili.
Naibu Waziri Ole Nasha amesema mashindano hayo yana umuhimu mkubwa hasa katika wakati huu ambao Nchi imeingia katika uchumi wa kati hivyo Teknolojia na ubunifu wa ndani ni muhimu sana ili nchi iendelee kuimarika na kukua zaidi.
" Kama mnavyojua wakati sisi tunapanda kutoka uchumi wa chini kwenda juu, maana yake kuna nchi zilishuka hivyo na sisi Kama hatutawekeza kikamilifu hasa katika teknolojia itakuwa ni vigumu kudumu katika uchumi wa Kati" amesema Mhe. Ole Nasha.
Amesema Serikali inathamini sana shughuli za ubunifu na itaendelea kuunga mkono kuhakikisha ubunifu wa Sayansi unakua nchini na kuleta tija kwa jamii.
Amesema ni muhimu kuendeleza bunifu za kiteknolojia kwa sababu baada ya kuingia uchumi wa kati Sasa ushindani utakuwa mkubwa Sana tofauti na tulivyokuwa katika uchumi wa chini kwani hakukuwa na ushindani mkubwa wa teknolojia.
Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof James Mdoe amesema mashindano hayo ya MAKISATU ni mojawapo ya mkakati wa serikali wa kuibua vipaji vilivyopo nchini na kuendeleza ubunifu walionao ili uwe msaada pia kwa Taifa.
Prof Mdoe amesema mashindano ya mwaka huu yameonesha ni jinsi gani kama Taifa tumebarikiwa kuwa na vipaji vingi ambavyo vikiendelezwa vitazidi kuifanya Nchi yetu iimarike pia kiuchumi kwani kuna vitu vitakua vikitengenezwa nchini na kuachwa kuagizwa nje.
Akizungumzia mashindano ya mwaka huu Prof Mdoe amesema jumla ya washiriki walioingia fainali ni 70 na wabunifu 21 walipatikana kutoka kila kundi na kuongeza kuwa kila mshiriki alieingia fainali katika wale 70 atakabidhiwa cheti.
Mashindano hayo ya MAKISATU yameshiriki makundi kutoka Shule za Msingi, Shule za Sekondari, Vyuo vya ufundi Stadi, Vyuo vya Kati, Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Vyuo Vikuu na wabunifu kutoka kwenye mfumo usio rasmi ambapo kauli mbiu ya mashindano hayo kwa mwaka 2020 ni " Sayansi teknolojia na ubunifu kwa uchimi wa Viwanda"
Mashindano ya MAKISATU yalianza mwaka 2019 na katika mashindano hayo yaliibua wabunifu 60 na wote wapo katika hatua mbalimbali za kuendelezwa katika bunifu zao.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akimkabidhi Hundi ya Sh Milioni Tatu, Frederick Uliki ambaye ni miongoni mwa washindi wa mashindano ya MAKISATU kwa mwaka 2020. Tukio hilo limefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya MAKISATU leo jijini Dodoma.
Wadau mbalimbali na washindi wa mashindano ya MAKISATU wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa zawadi kwa washindi hao ambapo mgeni rasmi alikua Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...