NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel, afanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya CCBRT iliyoko Msasani jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya CCBRT, Dk Mollel amesema kuwa anatambua mchangao wa hospitali hiyo katika kuwahudumia watanzania kwa upande wa afya.
“Nawafahamu CCBRT na kazi mnazozifanya kwa muda mrefu sasa, nawapongeza kwa kazi nzuri, kama Serikali tunatambua mchango wa hospitali hii katika kuwahudumia watanzania, leo nimefika kusalimia kidogo lakini naahidi kuja rasmi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ili tuweze kupata wasaa wa kujadilina kwa kina juu ya kazi zenu”. Amesema Dk. Mollel
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi
amemshukuru Dk. Mollel kwa kufika katika Hospitali ya CCBRT, na kumueleza ambavyo taasisi yake inanufaika na ubia kati yake na serikali tangu kuanza kwake hadi hapa ilipofikia.
“Kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu wa CCBRT napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali yetu kupitia Wizara ya afya tumekuwa tukipata msaada na ushirikiano mkubwa kutoka serikalini kwa hili, nasema asante sana na naomba utufikishie salam zetu kwa dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalim na watendaji wake wote”. Amesema Brenda
Hata hivyo Katika ziara isiyo rasmi Naibu waziri, amekutana na kusalimiana na uongozi wa hospitali hiyo huku akiwapongeza CCBRT kwa kazi nzuri pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel jijini Dar es Salaam leo alipotemelea Hospitali ya CCRBT.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa hospitali ya CCBRT.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Godwin Mollel akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi alipotemelea katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...