NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
TAASISI
ya Mfuko wa Emerson's Zanzibar Foundation (EZF) inatarajiwa kutangaza
matokeo ya uhakiki wa filamu 21 zilizowaswilishwa kwenye tunzo ya
filamu iliyokusudiwa kuendeleza na kukuza Vipaji vya Vijana wa
Kizanzibari wanaotengeneza filamu.
Akitoa
taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, Mwenyekiti wa Mfuko wa Wakfu wa
Emerson's Zanzibar Foundation, Said el-Gheithy alisema Wadhamini wa
Bodi ya mfuko huo EZF ulipokea jumla ya filamu 21 kutoka Unguja na Pemba
zilizoletwa katika tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka. Kati ya hizo
filamu Nane (8) pekee ndio zilizokidhi vigezo na sifa zilizowekwa.
"Mwaka huu tunatoa tunzo ya tano....
Filamu
21zilizoandaliwa na Vijana wa Kizanzibari kutoka Unguja na Pemba, nane
pekee ziliweza kupenya kwenye mchujo, na kuhakikiwa na Jopo la Majaji
katika hatua ya mwisho. Matokeo yatatangazwa Julai 4 mwaka huu hapa
Unguja." Alisema Mwenyekiti wa EZF, Said el-Gheithy.
Aliongeza kuwa:
"Bodi
ya Wadhamini ya Emerson Zanzibar Foundation imekuwa na utaratibu wa
kutoa tunzo hiyo mwezi wa Julai kila mwaka linapofanyika Tamasha la
Filamu za Kimataifa na za Nchi za Majahazi (ZIFF). Lakini mwaka huu
Tunzo hiyo itafanyika kupitia mitandao ya kijamii.
"Tunzo ya Tano kwa mwaka huu itafanyika mitandaoni kutokana na janga la Kirusi cha Covid-19.", alimalizia Said el-Gheithy.
Kwa
upande wake Meneja Mwandalizi wa shughuli za Tunzo hiyo, Salma Adim
alieleza kuwa tayari majaji wamekamilisha kuzikhakiki filamu hizo. Sasa
inasubiriwa kutangazwa matokeo.
"Filamu
zilizotengenezwa na Chipukizi ndio kauli mbiu ya mwaka huu. Hivyo basi
katika filamu hizo 21 ni nane pekee zilizokidhi vigezo....... .",
alisema Salma Adim.
Salma
Adim aliwataja Majaji Sita ambao ni wabobezi waliohakiki filamu hizo.
Nao ni Helen Peeks, Bi. Maryam Hamdan, Lisenka Beetsra na Salum Stika
ambao walihakiki hapa Zanzibar. Majaji wengine, Vanessa Victor na Amil
Shivji wao walihakiki filamu hizo kwa njia ya mtandao (online).
Alizitaja filamu hizo zilizoingia Nane Bora ni:
'Mashaka', 'Kipaji', 'Urithi wa Mila', 'Youth Africa Life', 'Kijiji changu', 'Fikra yakinifu', 'Hofu ya Subira' na 'Tubadilike'.
Wadhamini
wa bodi hiyo wameeleza kuwa, Mpewa mstahiki atatunukiwa fedha, Milioni
Mbili (Ml.2), Tunzo maalum ya EZF na cheti cha ushiriki katika tukio
adhimu Mjini Unguja.
Tunzo hiyo imekuwa ikitolewa kila mwaka kuibua vipaji vya Vijana wengi Visiwani Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...