Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na baadhi ya wakina Mama,
walioshiriki katika kazi za muda mfupi za ujenzi wa majengo ya
Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya
ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina, kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma Bw. Rashid Mchata.

Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango, akimuuliza Mfamasia wa Hospitali ya Wilaya
ya Buhigwe mkoani Kigoma, Bw. Juma Lukanya kuhusu changamoto ya
Kitengo cha Dawa, ambapo aliomba makabati ya kuhifadhi dawa
alipotembelea hospitalini hapo mkoani Kigoma

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Viongozi wa Mkoa wa Kigoma na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya
Buhigwe mkoani Kigoma baada ya kumaliza kutembelea majengo ya hospitali
hiyo.

Moja ya majengo ya Hospitali ya wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma linavyoonekana kwa sasa.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe mkoani
Kigoma, Bw. Fredrick Kanyondwi, akielezea huduma zinazotolewa katika
Hospitali hiyo ikiwemo huduma ya Mama na Mtoto kwa Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, alipotembelea na kukagua ujenzi
wa Hospitali hiyo wakati wa ziara ya kikazi mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akitoa maagizo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Bw. Anosta
Nyamwoga, baada ya kutoridhishwa na ubora wa baadhi ya miundombinu ya
Hospitali ya Wilaya hiyo, alipotembelea na kukagua ujenzi wake.

Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Bw. Wilson
Bigambo, akimuongoza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango, (kushoto), kuangalia majengo ya hospitali hiyo ya Wilaya
alipotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa
kwa fedha za Serikali. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina.

Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango, akimsikiliza mgonjwa Bw. Lucas Lulomona,
aliyefika kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe mkoani
Kigoma
……………………………………………………………………
Na. Josephine Majula na Peter Haule, WFM, Kigoma
Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa
Kigoma kumsimamia ipasavyo mkandarasi anayejenga Hospitali ya Wilaya ya
Buhigwe mkoani humo, baada ya kutoridhishwa na ubora wa majengo
ikilinganishwa na kiasi cha shilingi bilioni 2.4
zilizotumika mpaka hivi
sasa kujenga moiundombinu ya Hospitali hiyo.
Dkt. Mpango
alitoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa
Hospitali hiyo ya Wilaya ambayo licha ya miundombinu yake kutokamilika
ipasavyo imeanza kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwezi Juni, 2020.
“Ubora wa
majengo hauendani na matarajio, inatakiwa iwe Hospitali ya Wilaya ya
Kisasa kabisa hivyo muongeze usimamizi wa Mkandarasi, nitarudi tena hapa
mwezi wa nane na mkandarasi afikishiwe salamu kuwa Waziri
hakufurahishwa na ubora wa kazi kwa kuwa nikirudi nitaangali pia na
thamani ya fedha kama fedha za wananchi zimewaletea kitu kinacholingana
na fedha tulizotoa”, alieleza Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango
alisema kuwa fedha ya wananchi haitakiwi kuchezewa kwa kuwa wanatozwa
kodi hivyo inatakiwa kurudi kwao kwa kuwaletea huduma ambazo zinafanana
na thamani ya jasho lao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina alisema atayafanyia kazi maelekezo ya
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mpango, na pia akamuomba kusaidia
kuwezesha mradi huo kukamilika ili utoe huduma stahiki kwa wananchi kwa
kuwa Waziri huyo amefika na kujionea hali halisi ya huduma zinazotolewa.
Aidha alimshukuru Dkt. Mpango kwa
kuendelea kufanya ziara katika Wilaya hiyo na kukagua miradi inayopatiwa
fedha na Serikali na kuchukua hatua zitakazowezesha kupata thamani ya
fedha za miradi.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe, Bw. Fredrick Kanyondwi, alisema kuwa
kiasi cha Sh. bilioni 2. 7 kilipokelewa kwa awamu nne na Halmashauri ya
Wilaya ya Buhigwe kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo imeanza
kutoa huduma kuanzia Juni, 2020 kwa kutumia miundombinu iliyopo wakati
ikisubiriwa kukamilika ili kutoa huduma kwa ufanisi.
Alisema ujenzi wa
majengo ya Hospitali yametumia mfumo wa Force Acount ambapo jengo la
Maabara limekamilika kwa asilimia 95, Mama na mtoto asilimia 87, utawala
asilimia 99, jengo la wagonjwa wa nje asilimia 99 na majengo mengine
kama la mionzi, jengo la dawa na kufulia ambayo kwa ujumla yametumia
takribani Sh. bilioni 2.4.
Bw. Kanyondwi
alisema kuwa bado kuna upungufu wa takribani Sh. milioni 200 baada ya
ya Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe kubaini upungufu wa Sh. milioni 500
ambapo mwezi Juni zilitolewa Sh. milioni Sh. milioni 300 kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi huo na kusalia shilingi milioni 200 ambazo
zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...